Askofu Desmond Tutu kuzikwa Januari Mosi mjini Cape Town


Mwanaharakati wa muda mrefu dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini Askofu Desmond Tutu aliyeaga dunia jana Jumapili atazikwa mnamo Januari Mosi mwaka 2022 katika mji wa Cape Town.

Taarifa hiyo imetolewa na wakfu wa kiongozi huyo wa kidini ambaye pia ni mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel aliyotunukiwa mwaka 1984 kutokana na dhima ya kupinga ubaguzi wa rangi chini ya utawala wa wazungu wachache nchini Afrika Kusini.

Wakfu wake umesema matayarisho yanafanyika kwa ajili ya wiki nzima ya maombolezo na kutoa salamu za mwisho kwa mwili wa mwanaharakati huyo aliyeheshimika duniani kabla ya mazishi mjini Cape



from MPEKUZI

Comments