Tafsiri 17 Kuhusu Kuota Ndoto Upo Shuleni Unasoma Au Upo Shuleni Unafanya Mtihani Wakati Ulishamaliza Shule Miaka Mingi Iliyopita
IMESIMULIWA NA Dokta Mungwa Kabili…………………………………0744 - 000 473.
Awali ya yote ujumbe katika ndoto yoyote ile huwa unapatikana MWISHONI mwa ndoto wakati ndoto inaisha na sio MWANZONI mwa ndoto,
KUHUSU KUOTA UMERUDI UTOTONI AU SHULENI UNASOMA WAKATI SHULE ULISHA MALIZA ZAMANI.
Hii ni ndoto ambayo imekuwa maarufu sana katika siku za hivi karibuni. Siku hizi karibu kila mtu mzima anaota ndoto hii. Sio mara moja wala sio mara mbili ni mara nyingi nyingi.
Wapo wanao ota ndoto hii walau mara moja au mbili kila mwezi, wengine huota mara moja kila wiki na wengine huota karibu kila siku. Wakati mwingine mtu anaweza kuota ndoto hii Zaidi ya mara moja ndani ya usiku mmoja na hali hiyo inaweza kujirudia mfululizo, yani mtu amelala tuseme saa nne usiku , saa sita usiku anaota ndoto hiyo, anastuka. Akilala tena anaiota ndoto hiyo hiyo.
NINI MAANA YA NDOTO HIZI MBILI ; KUOTA UPO SHULENI UNASOMA AU UPO UTOTONI NA KUOTA UPO SHULE UNAFANYA MTIHANI AMBAO ULISHA UFANYAGA MIONGO KADHAA ILIYOPITA AU MIAKA MINGI ILIYOPITA ?
Tuanze na ndoto ya kuota UPO SHULENI UNASOMA WAKATI WEWE ULISHAMALIZAGA SHULE MIAKA MINGI SANA IMEPITA.
Ulimaliza darasa la saba mwaka 1994 na kuendelea na masomo ya juu. Sasa hivi umeshakuwa mtu mzima mwenye watoto na pengine wajukuu kabisa. Lakini unalala usiku unaota ndoto umerudi shuleni katika darasa hilo hilo la saba au hata chini ya hapo. Upo katika mazingira ya shule ulio kuwa unaisoma. Katika ndoto yako hiyo mazingira ya shule yako huwa ni yale yale yaliyo kuwepo kipindi unasoma hata kama katika ulimwengu wa nyama yameshabadilishwa. Mfano kulikuwaga na miti mikubwa labda sasa hivi imeshakatwa. Kulikuwa na sehemu ya wazi na sasa hivi imejengwa madarasa mengine. Wewe katika ndoto yako utakuwa katika mazingira yale yale yaliyo kuwepo mwaka huo wa 94 wakati bado unasoma katika shule hiyo.
JE NDOTO HII INA MAANA GANI ?
Dhana iliyo jengeka miongoni mwa watu wengi katika jamii ni kwamba ukiota ndoto hii basi maana yake ni kwamba kuna watu wanakurudisha nyuma kwa kutumia uchawi. Yani kwa lugha nyepesi kuna watu wanakufunga kichawi ili usipate maendeleo. Uendelee kubakia hapo hapo ulipo na uzidi kurudi nyuma kimaisha.
JE TAFSIRI HII NI SAHIHI ?
Jibu langu ni NDIO na HAPANA. Ndio kwa maana ya kwamba ukiota ndoto umerudi shuleni inaweza kuwa ina maanisha kwamba kuna watu wanakufunga kwa lengo la kukurudisha nyuma kimaendeleo lakini HAPANA kwa maana ya kwamba si kila unapo ota ndoto umerudi shuleni basi tafsiri yake ni kwamba kuna watu wanakuroga kwa lengo la kukufunga ubaki hapo hapo ulipo na kukurudisha nyuma.
Ndoto hii ina tafsiri nyingi sana. Kuipa tafsiri moja tu kama watu wengi wanavyo amini ni kuto kuitendea haki ndoto hii na ulimwengu wa ndoto kwa ujumla wake.
Kama nilivyo dokeza hapo juu, ndoto hii ina tafsiri nyingi sana. Baadhi ya tafsiri muhimu kuhusu ndoto hii ni kama ifuatavyo ;
TAFSIRI NAMBA MOJA : UNAPEWA ONYO KUHUSU MWENENDO NA TABIA ZAKO AMBAZO ZINAKURUDISHA NYUMA KIMAENDELEO.
Ulevi, uzinzi na uasherati pamoja na anasa za dunia ni miongoni mwa tabia na mienendo ambayo inarudisha nyuma maendeleo ya watu wengi sana . kama wewe unajihusisha na tabia hizo hapo juu halafu ukawa unaota ndoto umerudi utotoni basi ni ishara kwamba tabia na mwenendo wako vinakurudisha nyuma kimaendeleo. Tabia na mwenendo wako ndio mchawi wako namba moja.
2.TAFSIRI NAMBA MBILI : NI ISHARA YA KUKUONDOA HOFU JUU YA JAMBO ULILO LIFANYA AU LILILO KUTOKEA AMBALO LIMEKUFANYA UWE NA HOFU KUBWA SANA KATIKA MAISHA YAKO.
Mfano umekutana kimwili na mtu bila kutumia kinga halafu baadae ukasikia mtu huyo aliwahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na muathirika, jambo hili linaweza kukupa hofu kubwa sana kwenye nafsi kiasi cha kukata tamaa ya kuishi duniani kwa kuamini na wewe umeathirika na mwisho wa siku unaweza kujiingiza katika tabia za hatari zaidi kama kuendelea kufanya ngono nzembe na watu mbalimbali huku ukiamini kwamba wewe ndio unawasambazia . Matokeo yake basi katika mchakato huo wa kuwaambukiza na kuwasambazia watu virusi, wewe ndio unaweza ukajikuta unaambukizwa. Malaika walinzi wako kwa sababu wana uwezo wa kusoma nyota yako na kujua mambo yatakayo kutokea mbeleni, wataanza kukupa ujumbe wa kukutoa hofu kwa njia ya ndoto. Ukiwa katika hali kama hii halafu ukaanza kuota ndoto umerudi utotoni basi maana yake ni kwamba jambo unalo lihofia halipo. Yani kwa suala la usalama wa damu yako, damu yako ni salama kama ilivyo kuwa miaka mingi iliyo pita wakati upo utotoni. Hapa malaika walinzi wako wanakuwa wameisoma nafsi yako ambayo inatamani siku zirudi nyuma. Hivyo wanakujibu kwa njia ya ndoto kwa kukurudisha nyuma kwa njia ya ndoto.
Hapa malaika walinzi wako wakiona huelewi kwa njia ya ndoto, wataanza kukupa ishara nyingine za kawaida. Kwa mfano uta kuwa unatembea mjini mara unakutana na rafiki yako ambae mlisoma wote shule ya msingi na kwa mara ya mwisho mlionana miaka kumi iliyopita ( kipindi ambacho hukuwa na hofu kama uliyo nayo leo hii ). Unatoka hapo unaenda kupanda kwenye gari unasikia zinapigwa nyimbo za miaka 25 iliyo pita wakati upo darasa la tatu nakadhalila . ( Ukiona hivyo basi jua unapewa taarifa kwamba jambo unalo lihofia halipo wala halijakutokea kwa hiyo usiwe na hofu yoyote kuhusu jambo hilo )
4.TAFSIRI NAMBA NNE : UNAPEWA ONYO USIRUDIANE NA MTU ULIE KUWA UMEACHANA NAE.
Ulikuwa na mke, mume , mchumba au mpenzi halafu mkatengana. Baada ya muda Fulani, mke, mume, mchumba au mpenzi huyo akakuomba mrudiane. Ukiwa katika mchakato wa kutaka kurudiana nae unaanza kuota ndoto umerudi shuleni au utotoni. Tafsiri ya ndoto hiyo ni kwamba endapo utarudiana na mke, mume, mchumba au mpenzi huyo basi jambo hilo litakurudisha nyuma sana kimaisha. Malaika walinzi wako kwa sababu wana uwezo wa kuona mambo yatakayo kutokea mbeleni wanakupa tahadhari hiyo kwa njia ya ndoto.
Sababu zinaweza kuwa mke, mume, mpenzi, au mchumba huyo ana laana na vifungo vya kimasikini vya ukoo, familia au kijiji. Ukifunga nae ndoa au ukiwa nae katika mahusiano ya kimapenzi maana yake na wewe unakuwa umeunganishwa kwenye laana na vifungo vyake.
Vile vile sababu zinaweza kuwa tabia za mwanaume huyo zitakurudisha nyuma kimaendeleo. Kwa mfano inawezekana wewe unafanya kazi au shughuli inayo kuingizia kipato ambacho unakitumia kukidhi haja zako na kuwasaidia familia yako halafu huyo mwanaume yeye hataki kuoa mwanamke ambae anafanya kazi. Yeye akikuoa atataka uwe mama wa nyumbani. Atakuachisha kazi na hatotaka ufanye biashara yoyote na anaweza kutumia fursa hiyo kukunyanyasa pia na mwisho wa siku utaishia kuachana nae huku ukiwa umepoteza muda wako mwingi sana ukiwa nae. NDIO MAANA UNAPEWA ONYO USIRUDIANE NAE.
5. TAFSIRI NAMBA TANO : NI ISHARA KWAMBA MARADHI YA KICHAWI YALIYO KUWA YANAKUSUMBUA YAMEPONA.
Kama ulikuwa umetupiwa maradhi ya kichawi na yakakutesa kwa muda mrefu halafu baadae ukapata tiba ya kuondosha maradhi hayo basi kuna uwezekano mkubwa sana kuota ndoto umerudi utotoni.
Hii maana yake ni kwamba, maradhi yako yote yameondoshwa na sasa umekuwa mpya. Umerudi kwenye upya., Kwa hiyo kama upo kwenye kundi hili halafu ukaota ndoto umerudi utotoni basi maana yake ni kwamba wewe umekuwa mpya.
6.TAFSIRI NAMBA SITA : NI ISHARA KUWA NYOTA YAKO ILIYO KUWA IMEIBIWA AU KUCHAFULIWA SASA IMERUDISHWA.
Kama nyota yako ilikuwa imechukuliwa halafu ikarudishwa basi kuna uwezekano mkubwa wa wewe kuota ndoto umerudi utotoni.
Hii maana yake umekuwa mpya. Nyota yako imekuwa swafi kama ulivyo kuwa mtoto mdogo. Ukiachilia mbali kurogwa, nyota ya mtu huwa ina haribiwa na zinaa. Unapo fanya zinaa una haribu nyota yako kwa sababu una unganisha nafsi( nyota ) yako na nafsi ( nyota ) ya mtu unae fanya nae zinaa. Katika ulimwengu wa kiroho, watoto wadogo ni alama ya nyota inayo ng’aa ama nyota iliyo kamilika, nyota safi.
Sasa kama nyota yako ilikuwa imechafuliwa, imekufa, imeshushwa, imefungwa au ime imechukuliwa ( imeibwa ) halafu ukarejesha nyota yako. Ukiota ndoto umerudi utotoni maana yake ni kwamba nyota yako iliyo kuwa imeibwa sasa imerudi. Na kama wewe ni mwanamke basi tunasema umerudi kwenye ubikira. Umekuwa swafi.
7. NI ISHARA KWAMBA PESA ULIYO IPATA HIVI KARIBUNI ITAISHA YOTE BILA WEWE KUFANYA KITU CHOCHOTE CHA MAANA : Kama umepata pesa nyingi hivi karibuni baada ya kusota kwa muda mrefu labda kupitia kilimo au uchimbaji madini halafu ukaanza kuota ndoto umerudi utotoni au shuleni basi kuwa makini sana na matumizi ya pesa zako kwani hiyo ni ishara kwamba pesa zako zitaisha zote hivi karibuni bila wewe kufanya jambo lolote la maana.
Malaika walinzi wako kwa sababu wana uwezo wa kusoma na kuona mambo yatakayo kutokea katika siku za usoni, wanakupa tahadhari kwa njia ya ndoto. Kama upo katika kundi hili hakikisha unafanya mambo yote ya msingi uliyo kusudia kuyafanya hapo mwanzoni endapo ungepata pesa ulizo zipata.
Kama ulipanga kununua, nyumba, ardhi, kufungua kampuni, nakadhalika basi fanya hivyo haraka sana kwani pesa zako zitaisha zote bila kufanya jambo la maana.
Mara nyingi ndoto hii huwatokea wale wanao pata pesa nyingi na kuingia kwenye maisha ya starehe pamoja na wale wanao pata pesa nyingi halafu wana iacha tu benki huku wakisubiri wapate pesa nyingine Zaidi ndio wafanye wanacho taka kukifanya.
Sasa hapa Malaika walinzi wako ambao wana uwezo kuona mambo yatakayo kutokea mbeleni wanajua kuwa pesa hiyo unayo itaka hutoipata leo wala kesho.
Itachukua muda mrefu sana. Kwa hiyo wanakutahadharisha kuwa pesa yako uliyo weka utaishia kuitumia kidogo kidogo hadi itaisha yote hivyo basi kama ulikuwa na biashara unataka kufanya basi anza kufanya sasa kwa pesa hiyo hiyo uliyo nayo.
8.TAFSIRI NAMBA NANE : UNA TAHADHARISHWA KUTOWEKEZA PESA ZAKO KWENYE BIASHARA MPYA AMBAYO UNATAKA KUIFANYA.
Umetoa pesa ya mtaji kutoka kwenye biashara yako moja na unataka kuiweka yote au karibu yote kwenye biashara nyingine halafu ukaona unaanza kuota ndoto upo shuleni au umerudi utotoni basi tafsiri yake ni kwamba, endapo utawekeza pesa zako kwenye biashara hiyo mpya basi pesa zako zitapotea kwani biashara hiyo haitokulipa.
Ukiwa katika kundi hili na ukawa unaota ndoto hizo, nakushauri ufanye mambo yafuatayo : Moja usiweke pesa zako kwenye biashara hiyo kabisa, endelea kufanya biashara yako ambayo umeizoea au kwenye hiyo biashara mpya weka pesa kidogo sana ambayo hata kama itapotea basi wewe huto ijutia sana.
9.TAFSIRI NAMBA TISA: NI ISHARA KWAMBA MPANGO UNAO TAKA KUUFANYA UTA KUSABABISHIA HASARA KUBWA SANA NA UTAKURUDISHA NYUMA SANA.
Kama kuna mpango wowote ambao unataka kuufanya halafu ukaanza kuota ndoto upo shuleni au utotoni basi hiyo ni ishara kwamba, mpango huo ambao unataka kuufanya utakuletea hasara kubwa sana katika maisha yako na kukurudisha nyuma sana kifedha na kimaisha. Mpango unaweza kuwa wowote, mfano kuacha kazi unayo ifanya na kufanya kitu kingine, kuoa, kumroga mtu nakadhalika.
11. KWA MTU ALIE BWETEKA NA KAZI AU SHUGHULI ANAYO IFANYA.
Anaweza kuota ndoto kama ishara kwamba kubweteka/kuridhika kwake kunamkwamisha na kumrudisha nyuma kimaisha na kimaendeleo.
12. NI ISHARA KWAMBA MUNGU AMEKUFANYIA/ATAKUFANYIA WEPESI KWENYE JAMBO UNALO MUOMBA
Kama upo kwenye kipindi kigumu cha maisha na una muomba Mwenyezi Mungu akufanyie wepesi kuhusu magumu unayo yapitia halafu ukaota ndoto umerudi utotoni basi tafsiri yake ni kwamba Mungu amejibu maombi na dua zako na kwamba mambo yako yatakuwa mepesi muda si mrefu.
Mtoto ni kiumbe ambae maisha yake ni mepesi kwa sababu kila kitu anapata kutoka kwa wazazi ama walezi wake. Kwa hiyo kama upo kwenye kundi hili basi shukuru kwa sababu mambo yako yanaenda kufanyiwa wepesi.
13. NI ISHARA KWAMBA TABIA YAKO YA UZINZI NA UASHERATI INAKURUDISHA NYUMA KIMAENDELEO
Hakuna tendo linalo chafua na kuharibu nyota ya mtu kama uzinzi na uasherati. Nyota ya mtu ikichafuka na kuharibika basi na mambo yake yatachafuka na kuharibika pia. Kama unajihusisha na uzinzi na uasherati halafu ukaota ndoto umerudi utotoni basi huo ni ujumbe kwamba, tabia yako ya uzinzi na uasherati inachafua na kuharibu nyota yako na inakurudisha nyuma kimaendeleo. Kwa hiyo unatakiwa kubadili mwenendo wako haraka iwezekanavyo.
14. NI ISHARA KWAMBA KUNA WATU WANA IBA MALI ZAKO AU MALI ZAKO ZINA TEKETEA.
Kwa mfano una miliki duka au maduka na kwenye duka au maduka yako umeweka wafanyakazi wa kusimamia duka lako. Ukiota ndoto umerudi utotoni basi ni ishara kwamba kuna watu wanakuibia mali za duka lako na hivyo kukurudisha nyuma. Mfano mwingine ni kama una lima mashamba au unafuga mifugo halafu ukaota ndoto hii ya utotoni basi jua kuna watu wanakufanyia hujuma kwenye mashamba yako au mifugo yako, hujuma ambazo zinakurudisha nyuma kimaendeleo.
Mfano mwingine ni kama upo nje ya nchi unayo ishi halafu unatuma pesa kwa ndugu, jamaa au rafiki zako waliopo nchini kwako kwa ajili ya kujenga nyumba yako na kuisimamia, kununua mashamba, mifugo nakadhalika halafu ukawa unaota ndoto ya utotoni basi ni ishara kwamba nyumba yako haijengwi na ulio wapa kazi hiyo wanakula pesa yako tu.
17. KWA MTU ALIYE LISHWA LIMBWATA KWA LENGO LA KUCHUNWA PESA NA MALI ZAKE : Anaweza kuwa anaota ndoto amerudi shuleni au utotoni ikiwa ni ishara ya kwamba anarudishwa nyuma kimaisha na mtu ambae amemlisha limbwata la mapenzi.
Tafsiri zipo nyingi sana lakini kwa leo hizi zinatosha.
KUOTA NDOTO UNAFANYA MTIHANI AMBAO ULISHA UFANYAGA MIAKA MINGI IMEPITA .
Ndoto hii ni tofauti na kuota ndoto umerudi shuleni. Ndoto hii ni tofauti kabisa na kuota ndoto umerudi shule.
Ndoto hii ina maana ifuatayo : MAANA YA NDOTO HII NI KWAMBA MTIHANI WA KIMAISHA ULIO PEWA, UMEUSHINDWA, KWA HIYO LAZIMA UUFANYE TENA MTIHANI HUO. Na usipo ufanya basi utaendelea kukuandama katika siku zote za maisha yako.
Kwa mfano wewe ni mwanaume, uliingia kwenye ndoa halafu baadae ukagundua kwamba mke wako ni mkorofi na sababu hiyo basi ukaamua kuachana nae na sasa unatafuta mwanamke mwingine ambae sio mkorofi.
Usicho kijua ni kwamba mwanamke huyo unae muona mkorofi aliletwa kwako kama mtihani ambao ulitakiwa kuufaulu. Mungu aliuleta mtihani huo kwako ili ujifunze jinsi ya kuishi na mke mkorofi . Sasa wewe mtihani huo umeufeli, umemfukuza mkeo kwa sababu mkorofi. Ni sawa na kuacha kuandika majibu ya mtihani kwenye chumba cha mtihani kwa sababu maswali magumu. Kitatokea nini? Utafeli mtihani huo. Na ukifeli mtihani wa kiroho lazima uurudie. Hakuna mjadala katika hilo.
Sasa basi ukiwa katika mchakato wa kutafuta mke mwingine ambae sio ‘mkorofi’ kama huyo ulie muacha, halafu ukawa unaota upo shule unafanya mtihani ambao uliufanyaga miaka mingi imepita basi jua kuwa una fahamishwa kwamba, unapoteza muda wako kujaribu kufanya mtihani ambao ulishaufeli kwa sababu hata kwenye mtihani huo utaenda kufeli pia.
Hii ni kwa wote wanawake kwa wanaume.
Ndio maana wapo watu ambao hawatulii kwenye ndoa moja. Ndani ya miaka kumi mtu ana ndoa tatu na zote wameachana kwa sababu zinazo fanana.
Mifano ipo mingi sana ila huu wa ndoa ni mfano ambao unaweza kueleweka kwa urahisi.
Ni matumaini yangu kuwa sasa umejua ni kwanini unaota ndoto ukiwa umerudi utotoni, upo shuleni unasoma au unafanya mtihani ambao ulisha ufanya miaka mingi imepita.
IMESIMULIWA NA Dokta Mungwa Kabili…………………………………0744 - 000 473.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment