Mti wa Lufwambo na Uchawi Katika Nguvu za kiume !!!

IMESIMULIWA  NA. DOKTA  MUNGWA  KABILI……..0744  000  473.

Mti  Wa  Lufwambo ama ufwambo  ni  mti  unao patika   porini. Mti  huu  unajulikana zaidi   kwa  sifa  moja kubwa, nayo  ni  kutoa  vijitunda  vidogo vigumu  vyenye  rangi  mbili  moja  ya nyekundu  na  moja  ya  bluu.

Mti  huu  una  faida  na  matumizi  mengi. Moja  kati ya  faida  za  mti  huu  ni kwamba, unasaidia  kutibu  maradhi  ya  bawaziri  na  majani yake yanaweza  kuchemshwa  na  maji na  kutumika  kama  chai  kwani  yanapo kuwa  mabichi  huwa  na  radha  tamu sana  kama  sukari.  Enzi  za  mabibi na  mababu  zetu  ulipotokea  ukame, watu walitumia  majani  ya  mti  wa lufwambo kutengeneza  chai.

Pamoja  na  kuwa  sifa  hizo  nzuri, mti  huu pia  una sifa  moja  mbaya  sana, ambayo ni  kutumika  na  wachawi kutengeneza  na  kusababisha  maradhi  ya  udhaifu katika nguvu  za  kiume .

Mti  wa  Lufwambo  na  Uchawi  Katika  Nguvu  za  kiume !!!
Wachawi  wana  uwezo  wa  kumsababishia  mwanaume  maradhi  ya  ukosefu wa  nguvu  za  kiume   kwa  kutumia  uchawi.

Moja  kati  ya  njia  zinazo tumika  na  wachawi  katika kutengeneza  na  kusababisha  maradhi ya  nguvu  za  kiume  ni  hii  ya  kutumia  mti  wa  lufwambo.

Njia  hii  ni  hatari  sana  na  idadi kubwa  ya  wanaume wenye  maradhi  ya  nguvu  za  kiume  yatokanayo  na  kurogwa  yametengenezwa  kwa  kutumia  njia  hii ya  mti  wa  Lufwambo.

Mtu alietupiwa  uchawi  huu  ataanza  kupungukiwa  na  nguvu  za  kiume  taratibu  taratibu na  mwisho  wa  siku  atakuwa  hana  uwezo  wa  kusimamisha  kabisa.

Jinsi  uchawi  huu  unavyo  fanyika, zinachukuliwa shahawa za  mwanaume  aliekusudiwa  zinachanganywa  na  matone saba  ya damu za  wanyama wawili  tofauti, mmoja  ni ndege  asie paa  mwenye  miguu  miwili  na  nyingine  ya  mnyama  mwenye  miguu  minne.

Vitu  hivyo  vinachanganywa  na  damu  ya  hedhi  ambayo  ilitoka wakati  mwanamke  yupo  usingizini  na  kisha  vinawekwa  kwenye  chungu  cheusi, kati kati  ya  njia  panda jike ( Njia  panda  jike  ni  makutano  ya  njia  nne )

Vitu  hivyo  vinachanganywa  na  dawa  maalumu  za  kichawi  halafu, unachukuliwa  msumari wa jeneza  wenye  kutu,  unachukuliwa  mzizi  wa  mti  wa  Lufwambo  ambao  una kuwa  umechimbwa  siku  ya  Jumanne  mchana  na  mchimbaji  anapo uchimba  hatakiwi  kuhema  wala  kivuli  chake  kugusa  mti.

Baada ya  mzizi  huu  kuchukuliwa,  unachukuliwa  msumari  wa  jeneza wenye  kutu, msumari  huu  ndio unatumika  kama  kalamu ya  kuandika jina  la  mwanaume  alie  kusudiwa  na damu zilizo changanywa  na shahawa  za  mwanaume  husika zinatumika  kama  wino  wa kuandika na  kupigia  mhuri.

Upande  mmoja wa  mzizi  huu  wa  lufwambo  litaandikwa  jina la mwanaume aliekusudiwa, halafu upande wa  pili  yataandikwa  maneno  ya kichawi  na  alama  maalumu  za  majini  wa  kaburini.

Kazi  ya  kuandika maneno  hayo itafanywa na  ajuza  ambae maziwa yake yameisha lala.

Zoezi  hili  likisha  kamilika, utachukuliwa  mti  huo  na   kuvishwa kipande  cha  sanda kilicho tumiwa  na  maiti,  utafungwa  vizuri  na  kisha  kwenda  kuzikwa  kwenye kaburi alimozikwa  mwanamke mzee  kwa muda wa  siku saba.  Wakati mti  huu  unazikwa, yatakuwa  yanatamkwa  maneno  maalumu  ya  kichawi.

Baada  ya  siku  saba  mti utaenda  kufukuliwa, halafu atauchukua  mchawi  mmoja  ambae  atajipaka  mafuta  ya  tunge  jike  na  kwenda  kuutega  barabarani ili  ukanyagwe  na  kuvunjika.

Ukiisha  vunjika  basi  atauchukua  mti  huo na  kuacha  sarafu ya  shilingi  mia moja  barabarani  hapo  na  kisha  kuurudi nao nyumbani.

Akifika  nyumbani  atachukuliwa  jogoo  mwenye   rangi  nyekundu ambaye  ata tamkiwa  maneno  maalumu  ya  kichawi na  kisha  kufungwa kwa  kamba  iliyo tengenezwa  kwa  sanda  iliyo  tumika .

Ikifika  saa  kumi  na  moja  alfajiri jogoo  huyo akiwika  mara tu  mchawi  atamchukua  na  kumchinja  hapo hapo  na  kisha  atachukuliwa  atachanganywa  na  huo mti ulio vunjwa  na  gari  kisha  ataenda  kuzikwa  kwenye  makaburi  yaliyo  sahaulika  alfajiri  hiyo hiyo.

Kitacho  tokea  baada  ya  hapo, ni  mwanaume  alie kusudiwa  kuanza  kupungukiwa  na  nguvu  za  kiume  taratibu.

Mwanzoni  anaweza  kudhani  ni  hali  ya  kawaida, labda  nguvu  zimepungua  kwa  sababu  ya  mawazo , kazi  nyingi  nakadhalika.

Baadae  tatizo litazidi kuongezeka  na  mhusika  ataanza  kutafuta  tiba  bila  mafanikio yoyote. Atatumia  tiba  na  tiba, atazunguka  kwa  madokta na  waganga  bila mafanikio  yoyote  na  mwisho  wake  atakata  tamaa, na  mwisho  wa  siku  atakuwa  hana  uwezo  wa  kusimamisha  kabisa na asipo pata tiba  sahihi  basi  hayo ndio yatakuwa  maisha  yake.

Hili  ni tatizo  linalo  wasumbua  wanaume  wengi  sana  duniani na  bahati mbaya  wengi  wao  hudhani  labda  linasababishwa  na  njia za  kawaida lakini  kumbe  wao wanakuwa  wamerogwa.

Utajuaje  kama  tatizo  lako ni  la  kawaida ama  la  kurogwa ?  
Zipo  njia  za  kitabibu  ambazo  hutumika  kujua  kama  tatizo  la  udhaifu  katika  nguvu  za  kiume  ambalo  linamsumbua  mtu  linatokana  ima  na kurogwa  ima  na  sababu  za  kisayansi.

Mwanaume  mwenye  tatizo  la udhaifu wa  nguvu  za  kiume  litokanalo  na  kurogwa  anashauriwa  kufanyiwa  dua  ama tambiko  maalumu  kwa  ajili  ya  kubatilisha  uchawi  huo  hatari kabla  mambo hayajaharibika  zaidi.

Ni  tatizo  ambalo  limevunja  na  linaendelea  kuvunja  ndoa nyingi  sana  kwa  sababu  inakuwa vigumu  sana  kwa  mwanamke kuendelea  kuwa mwaminifu  katika  ndoa  yake  kwa  mwanaume mwenye tatizo  kama  hili ambalo  huwa la  muda  mrefu  na linakuwa halina  dalili  yoyote  ya  kupona.

Nikiwa kama  Tabibu wa  Jadi  nimekutana  na  kesi nyingi  sana  za  namna  hii. Nimekuwa  nikipokea  malalamiko  kutoka  kwa wanawake  wengi sana  ambao wanajaribu  kutafuta  namna  ya  kuwasaidia  wanaume  zao kuondokana  na  tatizo  hili.

Sababu kubwa  ya wachawi kutumia  uchawi  huu  ni kulipa kisasi, kukomoa  ama  kuwatesa  tu wanandoa  pamoja  na  watoto  wao.

IMESIMULIWA  NA  DOKTA. MUNGWA  KABILI….0744  000 473


from MPEKUZI

Comments