Jaji Mkuu wa Mahakama asisitiza mshikamano kwa watumishi wa Mahakama

Na Faustine Gimu
Wafanyakazi wa Mahakama hapa Nchini wametakiwa kufanya kazi kwa bidii na kwa ushirikiano ikiwamo kuwashirikisha wafanyakazi na watumishi wa ngazi za chini ili kuleta tija katika kuwahudumia wananchi.

Wito huo umetolewa leo, February 10, 2020, Jijini Dodoma na Jaji Mkuu wa Mahakama Tanzania, Profesa Ibrahim Juma, Wakati akifungua Baraza la siku mbili la wafanyakazi wa Mahakama wanaokutana Jijini Dodoma kutathmini na kuweka malengo ya pamoja katika kuboresha ufanyaji kazi wao.

 Pia amehimiza kwa muhimili huo kujenga Utamaduni wa kutafuta maarifa na taarifa zitakazo wawezesha kufanya kazi kwa ubunifu katika kuhudumia wateja wao.

Amesema ili kufikia malengo waliojiwekea ni lazima wafanye kazi kwa bidii kubwa na  kushirikiana kutoka ngazi za juu hadi ngazi za chini ili kuwa na uelewa mmoja kila linaliendelea kila mmoja awe anafahamu.

"Nilitake baraza hili kufanya kazi kwa bidii na kwa kushirikishana kutoka ngazi za chini mpaka ngazi za juu, muwe ni kitu kimoja kwa maendeleo na kuhakikisha jamii inapata haki zao kwa wakati" amesema Jaji Mkuu, Prof. Ibrahimi Juma.

Ameongeza kuwa "Kama watumishi wa Mahakama tuwe na utaratibu wa mara kwa mara katika kutafuta maarifa na taarifa ili kwenda na wakati kwa sababu Dunia ya sasa inabadilika kila siku hivyo lazima tujue" amesema.

Amebainisha kuwa kwa sasa dunia imebadilika hivyo watumishi mnapaswa kuisoma ili kuweza kufanya kazi kwa haki badala ya kuonea watu na kuongeza kuwa masuala ya mtandao ni muhimu kuyajua kwa sababu masuala ya tejnolojia ipo juu.

Jaji Mkuu amesema kuwa hivi sasa kuna mabadiliko makubwa katika mahakama ambapo kuna wataalam wengi jambo ambalo linaweza kurahisisha katika muhimili huo.

Jaji Mkuu amesema katika mkutano huo wa siku mbili mada ambazo zitaongelewa zikawe chachu ya kuleta mabadiliko katika utendaji kazi katika mahakama hapa nchini.

Amesema kuna haja ya kuwashirikisha watumishi wa ngazi za chini kwa sababu Kuna wakati bajeti huwa inapanda na kushuka hivyo watumishi wanapawa kujulishwa kama bajeti inapanda na kushuka  ili wajue kama imepanda au kushuka na kuelezwa nini sababu ya kufiki hivyo.

"Hakuna sababu ya kuwaficha kuhusu mabadiliko ya bajeti na miradi inayotekelezwa, "amesema

Amebainisha kuwa majadiliano na mapendekezo ya wafanyakazi katika baraza hilo itasaidia kuendeleza mpango mkakati wa Mahakama Katika utekelezaji wa mambo waliojipangia.

Pia amesema kuwa kwa Sasa ndani ya muhimili huo Kuna mabadiliko kwani kwa Sasa wanaowataalamu wa kada mbalimbali wa ndani Jambo ambalo Lina lahisisha utendaji kazi wa muhimili huo.

" Kwa Sasa tunawalaalamu mbalimbali wa ndani Kama Tehama,usimamizi wa maboresho, uhandisi, utunzaji wa kumbukumbu, uchumi na nyingine nyingi" amesema.


from MPEKUZI

Comments