Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara maarufu Jacqueline Wolper amemwaga povu baada ya tetesi kusambaa anatoka kimapenzi na msanii mkongwe wa Bongo fleva Mr. Nice.
Siku chache zilizopita Wolper na Mr. Nice walionekana pamoja wakila bata Kwenye club moja Nairobi nchini Kenya huku wakionyesha kuwa na ukaribu fulani.
Kwenye video ambayo iliwekwa Mtandaoni na Jacqueline Wolper iliwaonyesha wawili hao wakila bata yaani Wolper akivuta shisha huku Mr. Nice akinywa pombe ambapo watu mbalimbali walidai huenda wanatoka kimapenzi.
Baada ya Tetesi hizo za Mahusiano gazeti la Risasi lilimtafuta Wolper kwa njia ya simu akiwa nchini Kenya na kumuuliza kuhusu ukaribu wake na Nice ambapo alisema ni wa kawaida tu na wako karibu kwa sababu bosi wao ni mmoja.
"Watu wajue sisi tupo kikazi zaidi kwani kuonekana na mtu ni lazima awe mpenzi wako? Si lazima, huyu ni kaka yangu na bosi wetu ni mmoja, projekti yetu ikiwa tayari tutaitangaza itajulikana tu lakini kwa sasa bado ni mapema kuitangaza”.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment