Baada ya Dogo Janja kudai kuwa Rayvanny hajui kuvaa, muimbaji huyo amejibu hilo.
Rayvanny amesema kuwa Dogo Janja anakosea kusema hivyo kwani kuna tofauti kati ya mtu kujua kuvaa na mtu kupendeza.
“Kuna tofauti kati ya kuvaa na kupendeza, mtu akikuambia hujui kuvaa, anakosea, labda akuambie hujui kupendeza,” amesema.
“Cheni yake ambayo anaivaa sasa hivi, aliivaa Dully Sykes kwenye wimbo wa Sugar Mami. Kwa hiyo ukija kusema eti una uwezo wa kumvalisha Rayvanny hajui kuvaa, no!, unanikosea heshima kwa sababu mimi nimeenda sehemu nyingi nimeona watu wanavaa vitu tofauti,” Rayvanny ameiambia Wasafi TV.
Rayvanny ameongeza kuwa Dogo Janja kudai yeye ndiye anapendeza kuliko wasanii wote Bongo si kweli. Kwa haraka haraka amewataja wasanii ambao anaona wanapendeza ambao ni Jux, Diamond, Ben Pol, Chege na Harmonize.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment