Mume na Mke Wateketea kwa Moto.....Ni Baada ya Mwanaume Kufunga Mlango na Kisha Kuwasha Moto

Mume na mke, wamefariki dunia leo Juni 26 baada ya mwanaume huyo, kufunga mlango wa nyumba kwa ndani, kisha kutia moto nyumba hiyo.

Imeelezwa kuwa, tukio hilo limetokea, usiku wa saa saba, mnano Juni 25 katika eneo la Kilimahewa, Mailimoja, Kibaha.

Uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa, chanzo cha tukio hilo ni wivu wa kimapenzi.

Kamanda wa Polisi Mkoani Pwani Jonathan Shanna amemtaja mwanaume huyo kuwa ni Hussein Zaid (58) na mwanamke ambaye amefariki katika tukio hilo ni mke wake mdogo, Zainabu Juma (42).

“Siku ya tukio hilo Hussein alijaribu kujiua akiwa amejifungia ndani ya nyumba yake pamoja na mkewe huyo kwa kuzikusanya nguo zilizokuwa humo na kuziwasha moto kwa kutumia kiberiti,” alisema Kamanda Shanna na kuongeza:

"Kabla ya kutekeleza tukio hilo kwanza alijaribu kumchoma mke wake huyo kwa kisu na alipoona hajafanikiwa ndipo alipoamua kuichoma moto nyumba wote wawili wakiwa ndani.”

Ameongeza kuwa baadhi ya majirani walifika kutoa msaada na kuwajulisha Polisi ambao walifika eneo hilo.

“Hata hivyo, licha ya kuwaokoa wote wawili wakiwa hai, kisha kuwapeleka Hospitali ya Tumbi, lakini  walihamishwa Hospitali ya Muhimbili ambako walifariki dunia wakipata matibabu hospitali,” alisema


from MPEKUZI

Comments