Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ameondoka jana jioni kuelekea nchini Mauritania ambako atamuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwenye Mkutano wa 31 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika.
Mkutano huo wa siku 2, utakaoanza tarehe 1-2 Julai 2018, utafanyika kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Nouakchott ikiwa ni mara ya kwanza kwa nchi hiyo kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano wa AU.
Kaulimbiu ya mwaka huu ni Kushinda Vita Dhidi ya Rushwa chini ya Uenyekiti wa Rais wa Rwanda Mhe. Paul Kagame.
Ujumbe wa Makamu wa Rais unajumuisha Mheshimiwa Dkt. Balozi Augustine Mahiga (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki pamoja na viongozi wengine waandamizi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Afrika Mashariki.
Makamu wa Rais na ujumbe wake wanatarajia kurejea nchini Julai 5, mwaka huu.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment