Lori La Mafuta Lalipuka na Kuua Watu 9

Watu 9 wamefariki na magari 54 kuungua baada ya lori moja la mafuta kulipuka na kukamata moto barabarani wakati magari yakiwa kwenye foleni nchini Nigeria June 29.

Lori hilo liligongana na gari moja la abiria na kuanza kuwaka moto barabarani hapo wakati magari yakiwa kwenye foleni majira ya saa 11 jijini Lagos nchini Nigeria.

Inataarifiwa kuwa vifo kutokana na ajali hiyo vinategemewa kuongezeka kutoka Watu 9, huku moto huo ukiyafanya zaidi ya magari 50 yawe nyang'anyang'a.

Duru za kuaminika zinasema kuwa Watu waliofariki ni wale ambao walikuwa karibu na lori hilo ambalo lililipuka na kuwaka moto huku Watu wengine wakikimbia na kuacha magari yao kuokoa uhai wao.

Hata hivyo imeelezwa kuwa ajali za namna hiyo nchini Nigeria sio ngeni kwa maana huwa zinatokea mara kwa mara.


from MPEKUZI

Comments