Kigwangalla Apokea Taarifa Ya Awali Ya Tuhuma Za Mauaji Ya Tembo Zilizotolewa Na Kituo Cha Habari Cha ITV -London

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipokea taarifa ya awali ya uchunguzi wa tuhuma za mauaji ya Tembo katika Ikolojia ya Ruaha-Rungwa ambazo ziliripotiwa na kituo cha habari cha ITV-London mwaka 2017, kutoka kwa Mwenyekiti wa Kamati Maalum aliyoiunda kuchunguza tuhuma hizo, Kamishna Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova ofisini kwake Jijini Dodoma jana. 

Katikati ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Japhet Hasunga na Kaimu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Iddi Mfunda (kulia). 

Tuhuma hizo ziliwahusisha watumishi wa Serikali na Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo Duniani (UNDP) kupitia mradi wa SPANEST waliokuwa wakiufadhili.


from MPEKUZI

Comments