Miswada mitano ya mwaka 2018 ukiwemo wa Sheria ya kuitangaza Dodoma kuwa makao makuu ya nchi imewasilishwa bungeni leo Ijumaa Juni 29, 2018.
Miswada hiyo iliyosomwa kwa mara ya kwanza leo na makatibu wa Bunge ni wa sheria mbalimbali (namba 2), sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali (Namba 3).
Mingine ni wa sheria ya bodi ya kitalaamu ya walimu Tanzania na muswada wa marekebisho ya sheria ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi wa mwaka 2018.
“Kwa mara ya kwanza tumesoma miswada mitano ambayo tutaifanyia kazi Bunge lijalo ikiwamo huu wa Dodoma. Tunawashukuru mawaziri na huu ulikuwa ni muswada ulioahidiwa kipindi kirefu lakini ulikuwa hauji,” amesema Spika Job Ndugai.
“Muswada huu wa mji wa Dodoma kamati ya Serikali za mitaa ndio mtaushughulikia, huu wa namba mbili na tatu tutaupeleka kamati ya katiba na sheria.”
Kuhusu bodi ya kitaalamu wa walimu amesema utapelekwa Kamati ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii huku ule wa Ubia na Sekta Binafsi na Umma ukipelekwa Kamati ya Bunge ya Bajeti.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment