Dk Mollel aunga mkono ushuru wa korosho Kutopelekwa kwa Wakulima

Mbunge wa Siha (CCM) Dk Godwin Mollel ameunga mkono uamuzi wa Serikali kufuta kifungu cha 17A cha Sheria ya Sekta ya Korosho ili kuruhusu ushuru unaotokana na mauzo ya korosho ghafi  nje ya nchi kuingizwa katika Mfuko Mkuu wa Serikali, kwamba kuitaifanya Tanzania kuwa ya viwanda.

Akizungumza leo Alhamisi Juni 28, 2018 katika mjadala wa Muswada wa Sheria ya Fedha wa mwaka 2018, Dk Mollel amesema, “hatukatai kuwa wakulima wamefanya vizuri katika uzalishaji.  Ila kwa utaratibu huu kutasaidia kuanzishwa kwa viwanda vya Korosho.

Amesema hata daraja la Mkapa limejengwa kwa fedha zilizotokana na mapato kutoka maeneo mbalimbali na si fedha za korosho, kuwashawishi wabunge kukubaliana na uamuzi wa Serikali.

“Tunaunga mkono mawazo haya, hayaendi kumnyang’anya pato mkulima bali yanaenda kuondoa watu wa kati na wanaopinga kuanzishwa kwa viwanda vya kubangua korosho,” amesema.


from MPEKUZI

Comments