Diwani wa Kata ya Kia (Chadema), Yohana Laizer ameendelea kusota rumande baada ya hakimu anayesilikiza kesi yake kutokuwepo mahakamani, ikielezwa kuwa yupo likizo.
Diwani huyo anatuhumiwa kwa makosa mawili ya kumbaka na kumpatia ujauzito mwanafunzi wa shule ya msingi Obrieni iliyopo Kata ya Kia Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro.
Jana Juni 29, 2018 kesi hiyo namba 152 ya 2018 ilipangwa kusikilizwa katika mahakama ya Wilaya ya Hai, lakini imeahirishwa kwa mara ya tatu kutokana na hakimu kutokuwepo mahakamani.
Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Wilaya ya Hai, Regina Mushi ambaye kesi hiyo kwa mara ya kwanza ilitajwa mbele yake, alisema hakimu mwenye mamlaka ya kusikilia kesi hiyo yupo likizo, kwamba yeye hana mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo mpaka pale hakimu huyo atakaporejea.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Julai 5, 2018 kwa ajili ya usikilizwaji wa awali.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment