16 Bora Za Kombe La Dunia 2018 Kuanza Jumamosi Hii kwa mchezo mkali kati ya Ufaransa na Argentina

Hatua  ya 16 Bora ya Kombe la Dunia inaanza Jumamosi kwa mchezo mkali kati ya Ufaransa na Argentina mjini Kazan, huku England ikimenyana na Colombia Julai 2.
 
Mechi za nyingine za 16 Bora ni kati ya Uruguay na Ureno Jumamosi pia, Hispania na Urusi, Croatia na Denmark, Jumapili, Brazil na Mexico, Ubelgiji na Japan na Sweden na Uswisi Julai 2 Jumatatu.
 
Hiyo ni baada ya mechi za makundi kukamilishwa jana, bao pekee pa Adnan Januzaj dakika ya 51 likiipa ushindi wa 1-0 Ubelgiji dhidi ya England kwenye mchezo wa Kundi G. 
 
Ubelgiji inamaliza katika nafasi ya kwanza kwenye Kundi G kwa pointi zake tisa, ikifuatiwa na England yenye pointi sita na zote zinafuzu hatua ya 16 Bora huku Tunisia na Panama zikiishia hapa.

Neymar ataiongoza Brazil katika mechi dhidi ya Mexico Jumatatu hatua ya 16 Bora Kombe la Dunia

Hali mbaya kwa Afrika, baada ya timu zake zote kutolewa hatua ya kwanza tu, kufuatia Senegal kuungana na Nigeria, Morocco, Misri na Tunisia kuaga mashindano hayo baada ya kufungwa 1-0  jana na Colombia katika mchezo wa Kundi H, bao pekee la beki, Yerry Mina dakika ya 74 Uwanja wa Samara Arena nchini Urusi. 
 
Timu zinazoaga mashindano haya ni pamoja na mabingwa watetezi, Ujerumani Saudi Arabia, Misri, Iran, Morocco, Peru, Australia, Nigeria, Iceland, Serbia, Costa Rica, Jamhuri ya Korea, Tunisia, Panama, Senegal na Poland.


from MPEKUZI

Comments