Je wewe ni msichana mwenye kipaji cha kuimba? Unahitaji kuendeleza kipaji chako cha kuimba lakini haujui uanzie wapi? Kama jibu lako ni NDIO basi HII NI HABARI NJEMA SANA KWAKO. Madusko dusko Entertainment Promotion ina hitaji wasichana watatu wenye vipaji vya kuimba .
Mmoja awe na uwezo wa kuimba sauti ya KWANZA vizuri , wa pili awe na uwezo wa kuimba sauti ya pili vizuri na wa tatu awe na uwezo wa kuimba sauti ya tatu vizuri. Kama akiwa na uwezo wa kuimba sauti zaidi ya moja au sauti zote tatu atakuwa amejiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kupata nafasi hii. Awe anaishi jijini Dar Es Salaam au Zanzibar. JINSI YA KUFANYA USAILI.
Tuma voice note ukiimba wimbo wowote uupendao kwenda namba 0745 433 595. Unapotuma voice note yako taja majina yako kamili, umri wako na mahali Unapo ishi. Kwa watakao chaguliwa wataunda kundi jipya la muziki na wataingia studio Mwezi wa nane kwa ajili ya kurekodi albamu ya muziki.. NB: usipige simu. Wewe tuma voice note yako pamoja na maelezo kama yalivyo andikwa hapo juu. Mwisho wa kupokea voice note ni Jumatatu tarehe 25 Julai 2022 saa tisa kamili alasiri. Watakao tuma voice notes zao mapema ndio watakao zingatiwa zaidi.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment