Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi Dkt. Pindi H. Chana (Mb), amemteua Bw. Imani Joel Kajula kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Chuo cha Taifa cha Utalii Tanzania (NCT) kwa kipindi cha miaka mitatu. Mhe. Balozi Dkt. Pindi H. Chana amefanya uteuzi huo kwa mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 5 (4) cha Sheria ya Wakala za Serikali Sura 245 kikisomwa kwa pamoja na Aya ya 2.2 ya Amri ya kuanzishwa kwa Chuo hicho cha Taifa cha Utalii. Aidha, amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Chuo cha Taifa cha Utalii Tanzania (NCT): –
- Prof. Wineaster Anderson, Prof. Mshiriki, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam – Shule ya Biashara;
- Bw. Matendo Bwire Manono, Wakili Mkuu II, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali;
- CPA. Suzana Steve Chaula, Mhasibu Mkuu, Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE);
- Bw. Enock Robert Wagala, Mkurugenzi wa Mipango, Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA);
- Bibi Gerwalda Florence Luoga, Mkurugenzi wa Utawala na Menejimenti ya Rasilimaliwatu, Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).
Uteuzi huu ni wa miaka mitatu kuanzia tarehe 12 Julai, 2022 hadi 11 Julai, 2025.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment