Na Mwandishi Wetu, Ufaransa
UBALOZI wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Ufaransa, umekutana na wadau wa Utalii mjini Paris kwa ajili ya kuonyesha na kufanya uzinduzi rasmi wa filamu ya 'Royal Tour', iliyoigizwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Aidha, tukio hilo lililofanyika Julai 8,2022 katika ukumbi wa Ubalozi lilihidhuriwa na Mhe. Tabia Maulid Mwita ambaye ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar .
Waziri Mwita alikuwa akiiwakilisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika katika maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani yaliyofanyika Makao Makuu ya UNESCO tarehe 7 Julai 2022.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment