Jeshi la Ukraine limefanya mashambulizi katika daraja moja la kimkakati linalotumiwa na Urusi kwa ajili ya kuyasambazia majeshi yake yaliyoko kusini mwa nchi hiyo silaha.
Haya yamefanyika wakati ambapo Urusi imeshambulia maeneo kadhaa nchini Ukraine kwa maroketi na makombora.
Naibu mkuu wa serikali ya Kherson aliyeteuliwa na Urusi Kirill Stremousov amesema jeshi la Ukraine limeishambulia daraja la Antonivskyi katika mto Dnieper.
Stremousov amesema daraja hilo halikuanguka ila lina mashimo yanayowia magari vigumu kupita.
Ameongeza kwamba majeshi ya Ukraine yametumia silaha za kutoka Marekani za HIMARS kurusha maroketi.
Mapema katika vita hivyo, majeshi ya Urusi yaliliteka kwa haraka eneo la Kherson lililoko kaskazini mwa rais ya Crimea ambayo Urusi iliiteka katika uvamizi wa mwaka 2014.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment