Rais Samia aipongeza Mwanamke Initiative Foundation kwa juhudi za kumkomboa Mwanamke

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (katikati) akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Mwanamke Initiative (MIF) uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar Juni 19, 2023, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Wengine pichani ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemad Suleiman Abdulla (wa pili kushoto), Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Lela Mohamad Mussa (kushoto), Mwenyekiti na Muanzilishi wa Taasisi ya Mwanamke Initiative (MIF), Mhe. Wanu Hafidh Ameir pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo, Mhe. Fatma Mwassa. Picha zote na Othman Michuzi.

=======  ======  =======

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameipongeza taasisi ya Mwanamke Initiative kwa juhudi kubwa inazofanya katika kumkomboa Mwanamke wa kitanzania hususani katika upande wa elimu. Pongezi hizo zimetolewa na Rais Samia katika uzinduzi wa taasisi ya Mwanamke Initiative Foundation (MIF) uliofanyika katika hoteli ya Golden Tulip Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Rais Samia amewapongeza sana MIF kwa kuweza kutazama changamoto ya ufaulu kwa watoto wa kike katika visiwa vya Zanzibar na kuja na suluhu ya kutaka kumaliza tatizo hilo ambapo takwimu zinaonyesha kumekua na ufaulu hafifu kwa watoto wa kike visiwani Zanzibar hali inayokwamisha maendeleo ya haraka kwa mtoto wa kike na jamii nzima kwa ujumla.
“Jambo linalofanya na wenzetu wa MIF ni jambo la kizalendo linalopaswa kuungwa mkono na wadau mbalimbali kwani sote tuna fahamu kuwa ukimwezesha Mwanamke umeiwezesha jamii nzima hivyo taasisi hii inakwenda kuikomboa jamii nzima kupitia juhudi ambazo inafanya kwa mtoto wa kike” alisema Rais Samia.

Rais Samia aliongeza kusema kuwa kuifungua MIF ni jambo moja laikini kutatua changamoto zilizopo ni jambo lingine, hivyo ameipongeza MIF kwa kuonesha nia ya dhati katika kutatua kama sio kumaliza changamoto zilizopo. Pia aliwashukuru Walimu wahitimu ambao bado hawajapata ajira kwa kujitoa na kuungana na MIF kujitolea kutoa mafunzo ya ziada kwenye kambi za wanafunzi wanao karibia kufanya mitihani yao, kwani hii imekuwa chachu ya kuongeza ufaulu visiwani Zanzibar.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu MIF, Fatma Mwassa alisema MIF kama taasisi, itajihusisha na ukombozi wa mwanamke kupitia uwezeshaji kielimu na afya na hata sekta ya kilimo. Aidha, MIF kupitia mpango mkakati wake wa miaka mitano inakusudia kuwa na kituo kitakachoshughulika na watu wenye changamoto za afya ya akili na ulemavu wa kiakili, eneo ambalo mara nyingi husahaulika na nguvu Nyingi kuwekezwa kwa watu wenye ulemavu wa viungo tu.

“Ni matamanio ya MIF kushirikiana na wadau wa ndani na nje ya nchi na kufanya kazi bega kwa bega  na wananchi wote ili kuunga mkono jitihada za Serikali katika kupambana na umaskini, ujinga na maradhi kupitia uwezeshaji wa wanawake” alisema Bi. Fatma ambae amekua Afisa Mtendaji Mkuu wa Kwanza wa Taasisi hiyo.
Pamoja na kuzinduliwa kwake, taasisi ya MIF tayari imefanikiwa kutekeleza miradi kadhaa ikiwemo kutoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi bora wawili wasichana ambao watasomeshwa mpaka pale watakapofika kikomo cha elimu yao. Sambamba na hilo MIF inatoa ufadhili wa masomo kwa wanafunzi 10 wanaoshika nafasi 10 za juu kupata masomo nje ya nchi (Scholarship) kwa wasichana. Mpaka sasa MIF imefanikiwa kuwapeleka wanafunzi zaidi ya 100 katika vyuo vya ufundi Tanzania Bara, lakini pia inakusudia kujenga vyoo 150 katika shule mbalimbali nchini ambavyo kati ya hivyo 75 vitajengwa Tanzania Bara.

Taasisi ya MIF inafanya kazi na wadau wengine mbalimbali ili kutimiza malengo yake na kupitia urabishi wake na mabenki  na taasisi nyingine binafsi, imeweza kukusanya kiasi cha shilling Bilioni 1.7 ambazo zitaelekezwa kwenye uendeshaji wa taasisi hii. Vilevile taasisi ya MIF imeingia mkataba na nchi ya falme za kiarabu (U.A.E) ambao hawa watatoa ufadhili wa takribani Bilioni 15 utakaokwenda kusaidia ujenzi wa kituo cha mafunzo cha Amali-VTC, kituo ambacho kitakwenda kutoa mafunzo ya amali kwa wahitimu 1,000 kila mwaka. 
Naye Mwenyekiti na Mwanzilishi wa MIF, Mh. Wanu Hafidh Ameir ambae ni Mbunge wa Viti Maalum visiwani Zanzibar alisema tangu utotoni ilikua ni ndoto yake kuweza kutoa mchango kwa wenye uhitaji katika jamii na ndipo lilipoanzia wazo la kuanzisha taasisi ambayo itakwenda kutoa msaada kwa jamii bila kujali uwepo wake binafsi ambapo lengo la taasisi hiyo ni kuona watoto wengi wa kike wanamaliza shule, wanafaulu na kujiamini kuendeleza maisha yao.

“ Sisi kama MIF milango yetu ipo wazi kwa kila mtu ambae anataka kuwa sehemu ya harakati hizi za kumkomboa mtoto wa kike na watoto wote kwa ujumla na kuona kwamba hawaishii njiani katika ndoto zao za maisha bali wanakamilisha ndoto zao na kuwa na mchango kwa jamii zao na Taifa zima kwa ujumla,” aliongeza Wanu.
Sambamba na kuboresha elimu kwa wanafunzi, MIF inakusudia kuinua viwango vya ufundishaji kwa kuendesha mafunzo ya walimu walio kazini. Kupitia programu ya 'MIF Fellows', taasisi ya MIF inakusudia kuinua viwango vya ufaulu, hususan Zanzibar, kwa Elimu ya Sekondari kwa wanafunzi kupata usaidizi wa kuyapata maarifa kupitia walimu wasaidizi walio katika mpango wa 'MIF Fellows'.

Aidha, Aidha, MIF inakusudia kuwasaidia wasichana waliokatiza masomo kutokana na sababu mbalimbali ili waweze kuendelea na masomo ya Ufundi na Sekondari kupitia Vyuo Vya Maendeleo ya wananchi (FDCs) na taasisi nyingine zenye kutoa mafunzo kama hayo, Bara na Visiwani.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya awali kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Mwanamke Initiative (MIF), Mhe. Fatma Mwassa wakati alipowasili kwenye hafla ya uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Mwanamke Initiative (MIF) uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar Juni 19, 2023, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakati hafla ya uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Mwanamke Initiative (MIF) uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar Juni 19, 2023, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Hemad Suleiman Abdulla akitoa salamu za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar wakati hafla ya uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Mwanamke Initiative (MIF) uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar Juni 19, 2023, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Mwenyekiti na Muanzilishi wa Taasisi ya Mwanamke Initiative (MIF), Mhe. Wanu Hafidh Ameir akizungumza wakati hafla ya uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Mwanamke Initiative (MIF) uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar Juni 19, 2023, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Mwanamke Initiative (MIF), Mhe. Fatma Mwassa, akizungumza wakati hafla ya uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Mwanamke Initiative (MIF) uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar Juni 19, 2023, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
 
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mhe. Lela Mohamad Mussa akizungumza wakati hafla ya uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Mwanamke Initiative (MIF) uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar Juni 19, 2023, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda akizungumza wakati hafla ya uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Mwanamke Initiative (MIF) uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar Juni 19, 2023, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama akizungumza wakati hafla ya uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Mwanamke Initiative (MIF) uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar Juni 19, 2023, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.






































--

from MPEKUZI

Comments