Rais Samia afanya uteuzi PPRA,Shirika la Mzinga na Baraza la Masoko ya Mitaji na Dhamana Tanzania


Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amemteua Dkt. Leonada Raphael Mwagike kuwa Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya mamlaka ya ununuzi wa umma (PPRA) , Dkt. Mwagike ni mtaalam wa ununuzi na ugavi Chuo Kikuu cha Mzumbe Morogoro

Uteuzi huo wa Dkt Mwagike utaanza tarehe 21 Julai, 2022 baada ya mwenyekiti aliyepo Balozi Dkt. Martern Lumbanga kumaliza kipindi chake cha pili tarehe 20 julai 2022

Rais Samia pia amemteua Luteni Jenerali Mstaafu Samwel Albert Ndomba kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Mzinga huku Jaji Mustafa Kambona akiteuliwa kuwa Mwenyekiti wa baraza la masoko ya Mitaji na Dhamana Tanzania kuchukua nafasi ya Jaji Fredinand Wambali ambaye aliteuliwa kuwa jaji wa rufani, uteuzi huu umeanza tangu Juni 2, 2022



from MPEKUZI

Comments