Na Amiri Kilagalila,Njombe
Jeshi la polisi mkoani Njombe linamshikilia aliyekuwa mwalimu wa mazoezi bwana Abel Bulugwe (21) kwa tuhuma za kumshawishi na kufanya naye mapenzi mwanafunzi wake wa darasa la sita (11) mjini Njombe aliyemtorosha kwa usiku mmoja huku akiwa na mtoto wa mwaka mmoja.
Akitoa ufafanuzi juu ya tukio hilo kwa mwanafunzi wa shule ya msingi Mkombozi kitendo kilichotafsiriwa kuwa ni ubakaji,kamanda wa polisi wa mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia June 4 katika mtaa wa Indundilanga.
"Mwalimu huyu alimaliza field katika shule hiyo akarudi chuoni kwao na kumaliza mafunzo ya ualimu,na tarehe moja mwezi wa sita akawepo kwenye haya maeneo ya Njombe,alionana naye huyo binti wakati akienda saloon na mdogo wake matokeo yake mazungumzo yalikuwa mengi na mwanafunzi huyu na baadaye akaenda naye sehemu alikofikia kwa rafiki yake na yeye alikuwa anatafuta fedha kwa ajili ya kurudi nyumbani kwao baada ya kumaliza shule katika chuo cha ualimu Tandala"alisema Kamanda Issa
Kwa upande wake mtuhumiwa amekiri kutenda kosa hilo huku akidai kuwa kabla ya kwenda naye nyumbani kwake binti huyo alimsindikiza nyumbani kwao huku binti huyo akikataa kuingia nyumbani kwao kwa madai anaogopa kwa kuwa amechelewa kurudi.
"Sikutarajia kama angekuja na kwa kweli sikutoa taarifa yeyote,usiku nilifanya naye mapenzi wakati mtoto mdogo naye alikuwa hapo hapo kitandan"alisema Mtuhumiwa Abel Bulugwe
Kwa wa wazazi wa binti huyo wamesema wamefanikiwa kumpata mtoto wao Mara baada ya kutoa taarifa kwa wananchi na viongozi walioanza kutoa ushirikiano huku wakisitishwa na kitendo cha mwalimu huyo kwenda kulala na binti yao huku wakimfanyia ukatili mtoto wao mdogo kwa kukosa maziwa ya mama.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment