Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amependekeza kufutwa ada kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita ili kuwapunguzia gharama.
Kauli hiyo ameitoa Jumanne Juni 14, 2022 bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya Serikali ya mwaka 2022/2023.
Dk Mwigulu amesema kwa sasa wanafunzi wa kidato cha tano ni takribani 90,825 na kidato cha sita ni 56,880 na mahitaji ya fedha ni Sh10 3 bilioni.
“Serikali itajipanga kuangalia namna ya kusaidia vyuo vya kati kadiri hali ya uchumi itakavyotengemaa. Ili kuwapunguzia gharama watoto hao kama Rais alivyoielekeza Wizara, napendekeza kufuta ada kwa wanafunzi wa kidato cha tano na sita. Kwa hatua hiyo, elimu bila ada ni kuanzia shule za msingi mpaka kidato cha sita,”amesema
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment