Jeshi la Ukraine lakiri askari wake wamefurushwa katikati ya mji wa Severodonetsk

 


Jeshi la Ukraine limesema,wanajeshi wake wamefurushwa katikati ya mji wa Severedonetsk, mji ambao kwa wiki kadhaa sasa unakabiliwa na mashambulizi ya Urusi katika eneo la mashariki mwa jimbo la Donbass. 

Mkuu wa majeshi mjini Kiev amesema wanajeshi wa Urusi wameshambulia katikati ya mji huo kwa kufyetua mabomu na kuwafurusha wanajeshi wa Ukraine waliokuwa wamebakia katika eneo hilo.

 Kwa mujibu wa hali inayoripotiwa kwenye eneo hilo, licha ya pigo kubwa kwa wanajeshi wa Ukraine, bado mapigano yanaendelea katika eneo la mji huo wa Severodonestk na kwamba bado Ukraine inadhibiti kiasi thuluthi ya mji mzima. 

Saa chache kabla ya ripoti hiyo, rais Volodymyr Zelensky alisema wapiganaji wanaoitetea Ukraine wanapambana kuilinda kila sehemu ya ardhi yake katika mji huo. Kufikia sasa imeelezwa kwamba Urusi inadhibiti asilimia 90 ya jimbo la Luhansk na inaendelea kusogea mbele kuuzingira kikamilifu mji wa Severodonetsk. 

Kiwanda cha kemikali cha Azot kilichoko kwenye mji huo pia kimeelezwa kuwa chini ya Urusi. Kwa mujibu wa maafisa wa Ukraine bado kuna raia wanaoendelea kujificha kwenye kiwanda hicho wakijikinga dhidi ya mashambulio ya anga.



from MPEKUZI

Comments