Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewaasa wanafunzi wa kozi ya awali ya askari Polisi kuendelea kuheshimu nafasi waliyopewa na serikali kuhudhuria mafunzo ya awali ikiwa ni sehemu ya ajira ya kulinda maisha ya watu na mali zao na hivyo kuitumia nafasi hiyo kwa kutokufanya mambo ya ovyo yatakayoharibu maisha yao ya baadae.
IGP Sirro amesema hayo akiwa katika Shule ya Polisi Tanzania, Moshi mkoani Kilimanjaro ambapo amewataka wanafunzi hao kuzingatia mafunzo wanayoyapata na kuto kuchezea nafasi waliyoipata kwa kufanya vitendo vya utovu wa nidhamu na kupelekea kufukuzwa mafunzo hayo.
Shule ya Polisi Tanzania maarufu CCP inazaidi ya wanafunzi elfu nne wa kozi ya awali ya askari Polisi ambao wanapata mafunzo ya uaskari Polisi kwenye shule hiyo.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment