Waziri Bashungwa aagiza watumishi 12 waliohama kwa kugushi barua kuchukuliwa hatua


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Innocent Bashungwa amemuagiza Naibu Katibu mkuu anayeshughulikia TAMISEMI, Ramadhani Kailima kuwafuatilia watumishi 12 mkoani Tanga waliogushi barua za uhamisho, ili warudishwe kwenye vituo vyao vya kazi haraka iwezekanavyo.

Pia ameagiza watumishi hao 12 wachukuliwe hatua za kinidhamu kwa kosa la kugushi nyaraka za serikali.

Waziri Bashungwa ametoa agizo hilo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kuhusu matokeo ya taarifa ya ukaguzi wa hesabu za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mwaka wa fedha wa 2020/2021


from MPEKUZI

Comments