Umoja wa Ulaya waruhusu kuendelea kununua gesi kutoka Urusi


Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya imeziruhusu nchi wanachama kuendelea kununua gesi kutoka Urusi lakini bila ya kukiuka vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Urusi baada ya nchi hiyo kuimavia Ukraine. 

Hata hivyo Halmashauri hiyo inazishauri nchi wanachama kutofungua akaunti za sarafu ya Urusi ya Rouble ili kulipia gesi. 

Halmashauri hiyo ya Umoja wa Ulaya ilitoa ushauri huo baada ya kikao chake cha faragha kilichofanyika hapo jana.

 Kampuni za nishati za Ulaya zimekuwa zinajaribu kutafuta njia ya kuthibitisha namna ya kuendelea kununua gesi kutoka Urusi baada ya rais wa urusi VladimrPutin kutaka wanunuzi walipe kwa kutumia sarafu ya Rouble. 

Urusi ilizikatia gesi Poland na Bulgaria baada ya kukataa kulipa kwa Rouble.
 



from MPEKUZI

Comments