Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha kuanzia Mei 19 2022 tunaendelea na opereshini maalumu ya kupambana na wahalifu wanaotumia Pikipiki maarufu kwa jina la “TATU MZUKA” ambapo wamekuwa kero kwa wananchi katika mkoa hususani jiji letu siku za hivi karibuni.
Katika operesheni hiyo jumla ya watuhumiwa 14 wamekamatwa ambao wamekuwa wakijihusisha na matukio mbalimbali katika mkoa ikiwemo uporaji kwa kutumia pikipiki.
Aidha katika Operesheni hiyo jumla ya pikipiki 12 zilikamatwa huku mbili kati ya hizo zilikuwa hazina namba za usajili badala yake zilikuwa na plate namba iliyosomeka R.I.P SCOBER.
Watumiwa hao wamehojiwa kwa kina na kukiri kufanya matukio ya uporaji, ukabaji na kujeruhi watu kwa kutumia pikipiki hizo katika maeneo tofauti tofauti katika mkoa huu na wametaja mtandao mzima wa wahalifu wanaoshirikiana katika matukio hayo.
Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama tunaendelea na operesheni kali ya kuwatafuta watuhumiwa wengine waliotajwa.
Nitoe wito kwa wananchi hususani wazazi na walezi kuendelea kuwapa malezi mema nakuwaonya vijana wao ili kuepusha kutojiingiza katika uhalifu na uvunjifu wa sheria za sheria za Nchi. Vile vile niwaombe wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu kwa Jeshi la Polisi ambazo zimefanikisha sana operesheni hii.
IMETOLEWA NA:
JUSTINE MASEJO-ACP
KAMANDA WA POLISI
MKOA WA ARUSHA
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment