Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makane Mbarawa amesema serikali Kupitia wizara yake itaendelea kusimamia utunzaji wa miundombinu ya usafiri inayojengwa katika maeneo mbalimbali nchini ili iwe na manufaa kwa wananchi kama ilivyokusudiwa.
Kwa upande wa wananchi na watumiaji wote wa miundombinu hiyo Profesa Mbarawa amewataka kuisaidia serikali katika ulinzi kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Profesa Mbarawa ametoa kauli hiyo mkoani Tabora
wakati wa uzinduzi wa barabara ya Nyahua hadi chanya yenye urefu wa kilomita 85.4 iliyojengwa kwa kiwango cha lami.
Amesema barabara hiyo itarahisisha usafiri na usafirishaji katika mikoa yaTabora na Singida pamoja na mikoa jirani na nchi jirani za Burundi na Rwanda.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment