Profesa Hosea aibuka kidedea urais TLS


Rais wa Chama cha mawakili Tanzania (TLS) Profesa Edward Hosea ameendelea kukitetea kiti chake cha urais kwa kuibuka mshindi kwa kupata kura 621.

Akitangaza matokeo hayo jijini Arusha  Mei 27 katika ukumbi wa mikutano wa AICC, Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi, Charles Rwechungura amesema kuwa, kura zilizopigwa zilikuwa 1,150 ambapo Profesa Hosea ameibuka mshindi dhidi ya wagombea wenzake ambao ni Harod Sungusia (380) na Jeremia Mtobesya (145).

Akizungumza mara baada ya kutangazwa mshindi, Profesa Hosea amemshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumtetea katika nafasi hiyo huku akiwashukuru wanachama hao kwa kumwamini na kumchagua tena kuwaongoza kwa mara ya pili.

"Mimi niseme tu Sasa kwa kuwa mmenichagua tuache kutegemea wanachama kutoa hela zao, na natanguliza kuwepo kwa uwazi kwenye swala la hesabu tutakuwa makini Sana katika maswala hayo na nawaahidi katika hilo," amesema.

Amesema kuwa, atahakikisha kila kamati inawajibika kwa wanachama wake, huku akiwataka kuwa kitu kimoja.

 



from MPEKUZI

Comments