Kampuni Ya Infinix Kuzindua Toleo Bomba Kabisa la Simu ya Infinix HOT 12 Kesho....Hii Itafunika Simu Zote, Zawadi Kibao za Papo kwa Papo Zitatolewa
2022 umekuwa Mwaka mzuri kwa kampuni ya simu Infinix, ndani ya kipindi kifupi Infinix imefanikiwa kuzindua Infinix Smart 6 Series na Infinix HOT 12 series ikiwa imetangulia HOT 12i na kufuatiwa na toleo la kwanza la series ya HOT Infinix HOT 12 kuwa na processor yenye speed kubwa Zaidi.
Bila kupoteza muda Infinix imezindua mkubwa wao Infinix HOT 12 kupitia @infinixmobiletz.
Kupitia mtandao wa kijamii @infinixmobiletz. Kampuni ya simu Infinix ilizindua Infinix HOT 12 ikiwa na sifa hizi;
• Chipset aina ya Mediatek Helio G85
• Kitunza kumbukumbu/Memory 128GB Rom na Ram ya GB4 na Ram ya niongeza GB3.
• Battery ya mAh5000 na Wat 18 ya usb type c.
• Display ya inch 6.82” 90Hz Refresh rate.
Kwa mujibu wa taarifa za ndani Infinix wakishirikiana na Tigo watazindua tena Infinix HOT 12 hapo kesho. Hili limekuja baada ya wateja kubaki gizani kuhusu swala la bei na upatikanaji wa bidhaa hiyo wateja kutofahamu wapi wanaweza kununua.
Pia simu hii inatarajiwa kuwa na mwaonekano/design ya kipekee kabisa huku ikiwa imeongezwa ulinzi kwa kuwa na mifumo ya kisasa zaidi ya usalama unaofahamika kama side finger print na mfumo wa uendeshaji wa Android 11.
Je nini chengine tutegemee kuona kutoka kwenye simu hii, tafadhali usikose kuwafatilia @infinixmobiletz. Infinix HOT 12 #FASTANDFUN.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment