Bunge limeidhinisha bajeti ya Sh trilioni 2.7 ya mapato na matumizi ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa (JKT) bungeni mjini Dodoma .
Akiwasilisha bajeti hiyo jana , Waziri wa Ulinzi, Stergomena Tax, amesema katika Mwaka wa Fedha 2022/2023, Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa imelenga kutekeleza mpango na bajeti kwa kuzingatia Dira na Dhima ya Wizara, Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, Mpango wa Tatu wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2021/22 – 2025/26), Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030 (SDGs).
Pia amesema bajeti hiyo imezingatia ilani ya uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2020, na muongozo wa maandalizi ya mpango na bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2022/2023.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment