Serikali Kuendelea Kuboresha Makazi Bora Kwa Wahudumu Wa Afya.


Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha makazi ya wahudumu wa afya nchini ambapo kwa Mwaka wa Fedha 2021/22 imejenga nyumba 176.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel alipokuwa akijibu swali la Mbunge Mhe. Nora Waziri Mzeru (Viti Maalum) aliyeuliza Mpango wa Serikali kuwajengea nyumba wahudumu wa kada mbalimbali za afya na kuboresha makazi.

Dkt. Mollel amesema kuwa kwa mwaka wa fedha 2022/23 Serikali itajenga nyumba 300 za kukaa familia 3 kwa kila nyumba.

Katika hatua nyingine Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Tulia Ackson ameipongeza Wizara ya Afya kupitia Naibu Waziri wa Afya kwa kujibu vyema maswali na kwa ufasaha.

"Niwapongeze sana Wizara ya Afya kwa majibu ya moja kwa moja kwenye swali lililoulizwa" amesema Mhe Tulia Ackson


from MPEKUZI

Comments