January Makamba Atoa Kauli Sakata la Mafuta


Waziri wa Nishati, January Makamba, amesema kwamba mtu yeyote mwenye taarifa ama uwezo wa kuisaidia nchi kuleta mafuta ya bei nafuu, afike ofisini kwake kwa ajili ya mazungumzo.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Aprili 13, 2022, Bungeni jijini Dodoma.

"Mtu yeyote, pahala popote, Mtanzania yeyote mwenye taarifa au uwezo wa kuisaidia nchi kuleta mafuta ya bei nafuu karibu sana ofisini hata leo ili tuzungumze hilo jambo, hatuwezi kung'ang'ania kitu kumbe kuna kitu kingine kitatusaidia zaidi, nchi hii ni yetu wote," amesema Waziri Makamba.

Aidha Waziri Makamba akongeza, "Niwahakikishie Watanzania kwa nchi yetu ukilinganisha na majirani zetu, mafuta ya kutosha yapo juu ya kiwango cha kanuni tulizoweka ya siku 15, mafuta yapo na serikali itahakikisha yanaendelea kuwepo ili uchumi usisimame,".




from MPEKUZI

Comments