Mfalme Zumaridi na wenzake wafikishwa mahakamani


Diana Bundala maarufu kama 'Mfalme Zumaridi' na wenzake 84 leo Alhamisi Machi 17, 2022 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza kusomewa maelezo ya awali katika mashtaka matatu ikiwamo usafirishaji haramu wa binadamu.

Makosa mengine ni pamoja na kusanyiko lisilo na kibali na kuzuia maofisa wa Serikali kutimiza wajibu wao.

Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani hapo saa 6:00 mchana mbele ya ya Hakimu mkazi Mwandamizi wa mahakama hiyo, Monica Ndyekubora.


from MPEKUZI

Comments