Mahakama Kuamua Kama Mbowe na Wenzake Wana Kesi ya Kujibu Leo


Mahakama Kuu Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi leo Februari 18, 2022 inatarajiwa kutoa uamuzi kama Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe pamoja na Washtakiwa wengine watatu wana Kesi ya Kujibu au Hapana

Februari 15, 2022 Upande wa Mashtaka katika Kesi hiyo ya Uhujumu Uchumi yenye Mashtaka ya Ugaidi ulifunga Ushahidi baada ya Shahidi wa 13 kumaliza kutoa Ushahidi wake

Mawakili wa Jamhuri walifunga ushahidi wao na leo Februari 18 Mahakama imeahidi kutoa uamuzi wa kama Watuhumiwa wana kesi ya kujibu au la!


from MPEKUZI

Comments