Dk.Chaula Aitaka Ngos Kushirikiana Na Serikali Kuimarisha Uchumi Na Ustawi Wa Wananchi


 Na WMJJWM, Tanga
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula ametoa wito kwa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kushirikiana na Serikali kuimarisha uchumi na Ustawi wa wananchi.

Dkt. Chaula akizungumza na Mashirika hayo katika Mkoani Tanga amesema Baraza la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NaCoNGO) ni moja ya chombo muhimu katika nchi hii kinachosimamia NGOs, hivyo kinatakiwa kisimamie vema Mashirika yake.

“KilaShirika lina majukumu lililokusudia, ikiwemo kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii, lengo Jamii ibadilike na kurudi kwenye maadili yake” amesema Dkt. Chaula.

Amesisitiza kila slShirika kuangalia sababu ya kujisajili, litekeleze majukumu yake na kufuata kanuni sheria na miongozo iliyopo, ikiwemo kuwasilisha taarifa za kila mwezi.

“Kwa hiyo tunapofanya kazi tunategemea matokeo ambayo kila mwananchi atafurahia uhuru wa nchi hii na Ustawi wa mtu mmoja mmoja utaimarika” Ameongeza Dkt. Chaula.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Tanga Saimon Mdende akiwasilisha taarifa ya shughuli zinazofanywa na Idara hiyo amesema mkoa unashirikiana kwa karibu na NGOs kutekeleza afua mbalimbali ikiwemo kielimisha Jamii madhara ya ukatili wa kijinsia na madawa ya kulevya.

Naye mmoja wa wamiliki wa NGOs ya Gift of Hope Foundation inayoshughulika na kutoa huduma ya ushauri nasaha kwa waathirika wa madawa ya kulevya Said Mbaga, amemueleza Katibu Mkuu malengo ya Taasisi hiyo ni kuhakikisha vijana hawaingii katika mkumbo wa kutumia madawa hayo na waathirika wanapata Huduma na kurudi katika hali zao za kawaida.

Awali, katika Mkutano huo Afisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri wa Wilaya ya Muheza, hiyo, Vije Mfaume alisema kwa mwaka 2021/22 Halmashauri imetenga jumla ya shilingi milioni 213 kutoka makusanyo ya ndani kwa ajili kutoa mikopo kwa wajasiriamali Wanawake, vijana na watu wenye Ulemavu na hadi sasa jumla ya sh. milioni 132 imetolewa.


from MPEKUZI

Comments