Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo Alhamisi, Februari 10, 2022 akiwa ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka wamemjulia hali aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mikumi mkoani Morogoro na msanii nguli wa kizazi kipya Joseph Leonard Haule (Prof. Jay) aliyelazwa hospital ya Taifa Muhimbili akiendelea na matibabu.
“Tumemuona Ndugu yetu (Prof Jay) hali yake inazidi kuimarika, tumshukuru Mungu lakini niwashukuru madaktari kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kumhudumia, pamoja na mchango huu wa kuwezesha matatibu lakini kwa Niaba ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan niwahakikishie tutaendelea kutoa kila aina ya ushirikiano katika kuhakikisha matibabu yanaendelea vyema huku tukiendelea kumuombea apone haraka” Amesema Chongolo.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment