Tanzania na Jimbo la Dallas la nchini Marekani zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika nyanja za utalii, michezo, uwekezaji pamoja na kubadilishana uzoefu katika masuala ya uhifadhi wa maliasili pamoja na uendelezaji Utalii
Makubaliano hayo yamefikiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro (Mb) pamoja na viongozi mbalimbali katika Jimbo la Dallas wakati walipofanya vikao vya ana kwa nyakati tofauti kwa lengo la kujifunza namna wanavyoendesha shughuli za utalii pamoja kukuza ushirikiano baina ya pande zote mbili
“Tumezungumzia masuala ya kuimarisha uhusiano wetu baina ya Tanzania na Jimbo la Dallas pamoja na kuangalia namna tunavyoweza kuliteka soko la watalii katika Jimbo hilo, tumejadili mikakati ya kuanza na watalii ambao ni wanafunzi wa vyuo vikuu katika jimbo hilo lengo likiwa ni kupata soko la uhakika la watalii wengi zaidi katika siku za usoni ” Amesema Waziri Ndumbaro
Akizungumza na Mkurugenzi wa Idara ya Utalii wa Jimbo la Dallas Liliana Rivera, Dkt. Ndumbaro amesema moja ya shabaha kubwa ni kuhakikisha kunaanzishwa ndege ya moja kwa moja ya kutoka Tanzani kwenda Dallas ambapo amesema itaweza kusaidia Watanzania ambao ni watalii kwenda Dallas na Watalii kutoka Dallas kutembelea Tanzania
” Tanzania imeshaanzxa mazungumzo na Uongozi wa Jimbo hilo ili kuhakikisha hilo linafanikiwa na hivi wiki lijalo Mkurugenzi wa Shrika la Ndege Tanzania (ATCL) atakuja Marekani kwa ajili ya kufanya mazungumzio hayo
Katika ziara hiyo pia, Waziri Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Mchezo wa Gofu nchini Marekani, Bruce Davidson ambapo Dkt.Ndumbaro ametumia fursa hiyo kuinadi Tanzania kuwa ipo tayari kuwa Mwenyeji wa mashindano makubwa ya mchezo wa gofu yatayohusishwa Wachezaji mahiri wa mchezo huo
“ Mchezo wa gofu ni mchezo unaochezwa na watu wenye fedha nyingi hivyo kuwa wenyeji wa mashindano hayo tutapata fursa ya. kutangaza vivutio vya utalii kwa gharama nafuu kwa sababu wachezaji wakubwa pamoja na watu mashuhuri watakuja Tanzania , kupitia umaarufu wao vyombo vikubwa vya habari duniani vitaambatana nao kwa ajili ya kuripoti yatakayojiri” ameongeza Waziri Ndumbaro
Aidha, Katika mazungumzo hayo Dkt.Ndumbaro wamekubaliana kutangaza vivutio vya utalii kupitia mchezo huo kwa kutumia vyombo vya habari vya kimataifa vitakavyotumiwa katika kutangaza mchezom huo
Katika hatua nyingine, Waziri Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Dallas Safari Club, Corey Mason ambapo katika mazungumzo hayo wamezungumza maeneo ya kushirikiana ikiwemo kukuza utalii wa uwindaji na kutoa vifaa vya kukabiliana na ujangili wa wanyamapori
Aidha, Katika mazungumzo hayo wamejadiliana masuala ya Uwekezaji ambapo Dkt.Ndumbaro amewaita Wawekezaji wa Marekani hususan Matajiri wa Jimbo la Dallas kuja kuwekeza Tanzani kwa kujenga mahoteli yenye hadhi ya nyota tano
Katika vikao hivyo vya Waziri Ndumbaro aliambatana na Balozi wa Tanzania nchini Marekani nchini Marerkani Dkt. Elsie Kanza pamoja na Ujumbe wa kutoka Tanzania akwemo Mwenyekiti wa Bodi ya TAWA, Brigedia Jenerali, Hamisi Semfuko, Mkurugenzi wa Wanyamapori, Dkt. Maurus Msuha, Kaimu Kamishna Uhifadhi wa TAWA, Mabula Misungwi na Afisa Mwandamizi, Segoline Tarimo
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment