Rais Samia Afanya Uteuzi Wa Viongozi Wawili


Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Mcha Hassan Mcha kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Taarifa iliyotolewa leo Jumanne Januari 18, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais- Ikulu, Jaffar Haniu imesema kuwa Mcha anachukua nafasi ya Msafiri Lameck Mbibo ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Madini.

Kabla ya uteuzi huo Mcha alikuwa Kamishna wa Udhibiti na Utekelezaji (Control and Enforcement) Makao Makuu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

“Mcha anachukua nafasi ya Msafiri Lameck Mbibo ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Madini” imesema taarifa hiyo na kuongeza

Pia, taarifa hiyo imesema kuwa Rais Samia amemteua Balozi Celestine Joseph Mushy kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Austria.

Balozi Muhy alikuwa Katibu Tawala Msaidizi, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.



from MPEKUZI

Comments