NECTA Yatangaza Matokeo....Yasema ufaulu kidato cha nne umeongezeka


Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Charles Msonde amesema jumla ya watahiniwa 483,820 sawa na asilimia 87.30 wamefaulu mtihani wa kidato cha nne wa mwaka 2021.

Dk Msonde ameibainisha hayo leo Jumamosi Januari 15, 2022 wakati akitangaza matokeo ya darasa la nne, kidato cha pili na nne.

Amesema kati ya watahiniwa 483,820 wasichana waliofaulu 218,174 sawa na asilimia 85.77 huku wavulana wakiwa 204,214 sawa na asilimia 89.00 wamefaulu

Katika matokeo hayo, Dk Msonde amesema shule ya Kemebos ya Kagera imeshika nafasi ya kwanza katika 10 bora kitaifa 

Shule 10 bora matokeo ya form 4
1. Kemebos Kagera
2. St. Francis Mbeya
3. Waja Boys Geita
4. Bright Future Girls
5. Bethel Girls Iringa
6. Maua Seminary KLM
7. Feza Boys DSM
8. Precious Blood Arusha
9. Feza Girls DSM
10. Mzumbe Morogoro.

Dk Msonde amesema Consolata Lubuva aliyekuwa akisoma St Francis ameibuka wa kwanza kitaifa katika orodha ya 10 bora ya watahiniwa waliofanya vizuri.

Watahiniwa 10 bora matokeo form 4

1. Consolata Luguva St.Francis
2. Butoi Kangaza -//-
3. Wllhemia Steven -//-
4. Cronel John -//-
5. Mary Ngoso -//-
6. Holly Lyimo - Bright Future
7. Brandina St.Francis
8. Imamu Feza Boys
9. Mfalme Madili Ilboru
10. Clara Straton St.Francis



from MPEKUZI

Comments