Mvua Na Upepo Mkali Waleta Maafa Mafia, Baadhi Ya Nyumba Zaangukiwa Na Miembe Na Minazi


Na Mwamvua Mwinyi Pwani,
Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amewataka wananchi wa Mafia kuwa na tabia ya kusaidiana kunapotokea changamoto athari mbambali ili kupunguza madhara yanayoweza kujitokeza.

Kunenge aliyasema hayo kwenye ziara  ya kukagua athari za zilizosababishwa na mvua kubwa pamoja na upepo mkali ambapo ambapo maafa yaliyojitokeza ni pamoja na kukatika kwa Tishari bandari ya kilindoni miti mikubwa kuangukia makazi ya watu pamoja na kaya zaidi 46 kuathiriwa na mvua hizo.

Alieleza, mkoa wa Pwani umekumbwa na maafa ikiwemo Mafia, Kibiti, Mkuranga, Rufiji,Chalinze nyuma 36 pamoja na madarasa mawili kuezuliwa mabati na Upepo mkali kule shule ya Makombe,na Kisarawe nyumba 100.

"Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini zimeleta maafa Mkoa hapa, tuendelee kusaidia pale inapotokea shida na Serikali itaangalia namna ya kutia nguvu yake."alifafanua Kunenge.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Mafia Martin Ntemo alieleza hatua walizochukua ni kufika eneo la tukio na kuunda timu ya kufanya tathmini ili kujua ukubwa wa maafa yaliyojitokeza.

Baadhi ya wananchi waliothirika na athari hiyo wameiomba Serikali iwasaidie hasa katika kuwapimia maeneo wanayoishi yasiyo rasmi ili waishi kwa usalama zaidi.

"Tunashukuru viongozi kutukimbilia kuja kutupa pole,kitongoji hiki hakijapimwa,tunaishi kiholela, Serikali ifanye mkakati wa kutupimia ili tuishi kama wengine kwenye maeneo rasmi "walisema.


from MPEKUZI

Comments