Masauni Aitaka UNHCR Kufuata Sheria, Mwakilishi Mkazi Mpya Ajitambulisha Kwa Waziri

Na WMNN, Dar es Salaam.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, amelitaka Shirikika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) nchini kufanya kazi kwa kuzingatia sera, sheria na vipaumbele vya Serikali katika utendaji wake.

Masauni amezungumza hayo jijini Dar es Salaam,katika Kikao na Mwakilishi Mkazi mpya wa Shirikika hilo Nchini, Mahoua Bamba Parums, ambaye alifika ofisini kwa Waziri huyo kwa lengo la kujitambulisha baada ya kuwasili nchini mwishoni mwa mwaka jana.

“Karibu sana Tanzania na pia nakupongeza sana kwa kuteuliwa katika nafasi hii, natumai kupitia Shirika lako hapa nchini tutafanya kazi vizuri kwa kuzingatia sera, sheria na vipaumbele vya serikali katika utendaji wako,” alisema Masauni.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi huyo, Mahoua, pia alimpongeza Waziri huyo kwa kuteuliwa kwenye nafasi hiyo kuiongoza  Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

“Nakupongeza Mheshimiwa Waziri kwa kuteuliwa kwa kuteuliwa kuwa Waziri na pia naipongeza Tanzania kwa ukarimu wake wa kuendelea kupokea na kuhifadhi wakimbizi kwa miaka mingi sasa na naomba muendelee kufanya hivyo,” alisema Mahoua.

Pia Mwakilishi Mkazi huyo alimuhakikishia Waziri kuendeleza ushirikiano katika shughuli za hifadhi ya wakimbizi na UNHCR itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuwahudumia Wakimbizi.



from MPEKUZI

Comments