NA MWANDISHI MAALUM, LAS VEGAS, MAREKANI.
WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro ameyapongeza makampuni zaidi ya nane [8] ya Kitanzania yaliyopo Nchini Marekani kwa kazi nzuri ya kuitangaza Tanzania kwenye sekta ya uwindaji wa kitalii kwa ki kushiriki katika mkutano wa 50 wa mwaka wa Uwindaji wa Kitalii ( Annual Hunting Convention)
Mkutano huo wa 50 wa mwaka wa Uwindaji wa Kitalii ulioandaliwa na Safari International Club International (SCI) umeanza leo na unafanyika katika Jiji la Las Vegas, Nevada nchini Marekani
Akizungumza Jijini hapa, Dkt. Ndumbaro amesema maonesho hayo yanatoa fursa kwa Tanzania yakiwemo Makampuni na viongozi na maofisa wa Serikali walioshiriki katika mkutano huo kujifunza na kuinadi Tanzania katika masuala ya Uwindaji wa Kitalii katika nyanja za Kimataifa
‘’ Katika maonesho haya zaidi ya mmakampuni 200 yanayofanya Biashara ya Uwindaji wa Kitalii kutoka kila kona ya dunia yapo hapa ikiwemo kutoka bara la Ulaya, Amerika, Afrika, lakini nchi za Canada na Marekani yenyewe” Amesisitiza Dkt. Ndumbaro
Dkt. Ndumbaro amesema maonesho hayo ni makubwa sana ambayo yanatoa fursa kwa nchi kujifunza sekta ya uwindaji wa kitalii kuwa ipo wapi sasa hasa kipindi hiki cha ugonjwa wa UVIKO 19.’’
Ameongeza kuwa ” Mimi kama Waziri mwenye dhamana na Utalii najisikia fahari kuona makampuni zaidi ya 8 ya Kitanzania yapo hapa yakiiuza Tanzania kwenye sekta ya uwindaji wa kitalii.
Dkt. Ndumbaro amesema Makampuni zaidi ya nane kutoka Tanzania kushiriki ni hatua nzuri, ” Huu ni ushahidi tosha kuwa Makampuni hayo yanafanya vizuri na yanakubarika Kimataifa lakini pia tumechukua fursa hii ya kuweza kukutana nao kwa ujumla wake lakini pia mmoja mmoja kuweza kuzungumza nao na kubadilishana mawazo.’’ Alisem Dkt. Ndumbaro.
Amesisitiza kuwa Mazungumzo aliyoyafanya na Makampuni hayo yametufundisha mengi ikiwemo kuanza kuingalia sekta hii ya uiwndaji wa kitalii namna utofauti kabisa, na kwamba Uwindaji ni sekta ya kipekee sana ambayo inaweza ikawa na mchango mkubwa katika uchumi wa nchi kama itachukuliwa kwa uzito unaostahili
Tumekubariana tutaendelea kujipanga kushiriki kwa siku zilizobaki kuiuza Tanzania lakini muhimu zaidi kuongea na waandaji wa maonesho haya na maonesho mengine ili katika safari ijayo Tanzania ishiriki kama nchi kwa umoja wake na kwa fursa kubwa zaidi ili kuuza utalii wa uindaji kwa Tanzania,
..tunashukuru kwa fursa hii ambayo bado inaendelea.’’ Alisema Dkt. Ndumbaro.
Kwa upande wake mmoja wa wanaoendesha biashara ya Utalii wa Uwindaji nchini Tanzania ambaye yupo kwenye mkutano huo, Bw. Michael Mantheakis amesema Maonesho hayo Wamekuwa wakihudhuria kila mwaka na kupata faida kubwa ya soko kutoka kwa wateja wanaofika kwenye mikutano hiyo.
“Mikutano hii ni muhimu sana kuhudhuria kwani tunakutana na wageni mbalimbali na bila kuhudhuria unakosa fursa kwani Mawakala (agent) na wateja wanafika hapa” lisisitiza
..Hapa kuna Washiriki wa kutoka nchi zote za Afrika hivyo usipohudhuria Mkutano huu utakosa soko. Hapa ndipo tunapokutana na wageni wetu tunapata faida ya kuweza kuendesha safari zetu, wateja na Mawakala wanapata fursa ya kutufanyia usahili na pia wanaona jinsi tunayonadi bidhaa zetu’ alisema Michael Mantheakis.
Mkutano huo umeanza rasmi tarehe 19 Januari, 2022 na kufunguliwa rasmi tarehe 21 Januari 2022 katika Jiji la Las Vegas, Nevada nchini Marekani ukiwa na lengo ya kuwakutanisha watunga sera na wafanya maamuzi katika ngazi za juu kutoka nchi mbalimbali duniani kuweza kujadili masuala ya kisera katika kuendeleza sekta ya uwindaji.
Katika Mkutano huo, Dkt. Ndumbaro anazinadi fursa za uwekezaji za uwindaji wa kitalii zilizopo nchini Tanzania kwa lengo la kuwawezesha Matajiri wakubwa duniani kuchangamkia uwekezaji huo uliopo nchini Tanzania
Kupitia Mkutano huo Tanzania itaweza kuongeza uelewa zaidi katika masuala ya kisera na maamuzi katika kuendeleza sekta ya uwindaji wa kitalii nchini
Katika msafara huo, Waziri Dkt. Ndumbaro aliambatana na Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Dkt. Maurus Msuha, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TAWA, Meja Jenerali, Hamis Semfuko, Kaimu Kamishna Uhifadhi wa TAWA, Mabula Misungwi,
Mwingine ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Misitu Tanzania (TAFF) Lulu Ng’wanakilala pamoja na Afisa Mhifadhi Mkuu wa Wanyamapori wa kutoka TAWA, Segolin Tarimo
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment