Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro, amewavalisha nishani maofisa, wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali 123 waliotunukiwa nishani na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe Samia Suluhu Hassan.
Akisoma taarifa ya kuvisha nishani hizo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Mihayo Msikhela, amesema kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi kwa mamlaka aliyopewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, ametunuku nishani ya miaka 60 ya uhuru, nishani ya utumishi uliotukuka na nishani ya utumishi mrefu na tabia njema.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment