Gari la Wanahabari Lagongana na Hiache....Watu 14 Wafariki


Watu 14 wakiwamo waandishi wa habari saba wamefariki dunia baada ya gari la waandishi wa habari iliyokuwa kwenye msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza (RC), Robert Gabriel kugongana na gari ya abiria aina ya Toyota Hiace  katika eneo la Nyamikoma wilaya ya Busega Mkoani Simiyu.

Mkuu wa Wilaya ya Busega (DC), Gabriel Zakaria amethibitisha kutokea vifo hivyo.Amesema kati ya vifo hivyo kuna vifo vya waandishi wa habari wanne na dereva wa waandishi na watu wengine sita walifariki papo hapo

Ameongeza kuwa majeruhi waliopelekwa kwenye kituo cha afya cha Nasa, watatu wamefariki dunia na kufanya idadi ya waliofariki kufikia 14.



from MPEKUZI

Comments