Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM imepitisha jina pekee la Dk Tulia Ackson kuwa mgombea wa kiti cha Spika kilichoachwa wazi na Job Ndugai aliyejiuluzu nafasi hiyo Januari 6, 2022.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Januari 20, 2022 kwenye ukumbi wa White House Dodoma, Katibu Mwenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka amesema Kamati Kuu imepitisha jina moja la Dk Akson kati ya majina 70 ya makada wa CCM waliochukua na kurejesha fomu.
Utaratibu wa CCM ni kupeleka majina yasiyozidi matatu kwenye kamati ya wabunge. Wanaweza kupeleka moja au mawili au matatu.
Dk Tulia anakuwa mwanamke wa pili kuwa Spika kama atachaguliwa na wabunge.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment