TCRA Yakisimamisha Kipindi cha Shule ya Uongozi cha Mbunge Humphrey Polepole


KAMATI ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kipindi cha Shule ya Uongozi cha Mbunge Humphrey Polepole kinatolewa pasipo kuzingatia misingi, sheria na kanuni za huduma ya utangazaji huku kamati hiyo ikisimamisha kipindi chake cha Shule ya uongozi na kumpa masharti ambayo anapaswa kuyatimiza ili kirudi hewani.

Akisoma hukumu hiyo, baada ya kusikiliza upande wa Kamati na Upande wa Utetezi, Mwenyekiti wa Kamati, Habbi Gunze amesema maudhui ya kipindi cha shule ya uongozi yalikuwa ni ya upotoshaji na yanayoweza kusababisha taharuki kwa wananchi.

“Kuhusu kuwapanga wamachinga, Humphrey Polepole Online TV iliwatuhumu viongozi wa Serikali kuhusu kutofuata maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu ya kuwapanga vizuri wamachinga. Kituo hiki kimevunja kanuni na maadili ya uandishi na utangazaji kwa kutowapa nafasi viongozi hao kutoa ufafanuzi juu ya tuhuma alizotoa.

“Polepole alitoa maneno ya uongo na udharirishaji kwa viongozi akisema ni waoga na hawajitokeizi kutoa ufafanuzi kuhusu deni la Taifa bila kuwapa nafasi viongozi hao kufafanua madai yake wakati viongozi waandamizi wa serikali akiwemo Waziri wa fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba mwezi Juni alisema bungeni kuwa deni la taifa ni himilifu.

“Katika utetezi wake alisema amejikita katika utoaji wa elimu tu bila kuzingatia mizania na kwamba TV yake si kama vyombo vingine vya habari vinavyotoa maudhui ya habari, yeye anatoa elimu tu. Pia alidai kanuni hazijitoshelezi kwani hazielezi kwa mtu anayetoa maudhui ya elimu afanyeje, jambo ambaloi si kweli kwani kanuni zinajitosheleza na zinatoa mwongozo wote.

“Kamati imebaini kuwa Polepole TV haina waandishi wenye taaluma ya uandishi wa habari hivyo kukikua misingi ya uandishi na imemuelekeza ahakikishe anazingatia uchaguzi wa maneno yenye sitaha, kuzingatia misingi, kanuni na maadili ya utoaji maudhui mtandaoni.

Maamuzi ya Kamati

Kama imejiridhisha kuwa Polepole TV imekiuka shria za mawasiliano kwa njia ya kieletroniki, hivyo kwa mujibu wa kifungu cha 44, kifungu kidogo cha kwanza, sehemu G cha sheria ya mamlaka ya mawasiliano ya Tanzania, sura ya 172, na marejeo yake ya mwaka 2017, na kanuni ya 21, kanuni ndogo ya tatu na sehemu A ya kanuni tajwa hapo juu, Kamati inatoa adhabu zifuatavyo.

  1. Kituo kinapewa onyo kali.
  2. Kipindi cha Shule ya Uongozi cha Humphrey Polepole TV kusimamishwa kwa muda mpaka pale atakapofanya yafyatayo.
  • Kuwa na wafanyakazi wenye taaluma ya uandishi wa habari na utangazi na kuleta tija na ufanisi katika vipindi vyake.
  • Kuhakikisha vipindi vyake vyote vinazingatia sheria, misingi na kanunia za uandishi na utangazaji wa habari pamoja na masharti ya leseni yake.

“Baada ya kuzingatia maelekezo hayo Kituo cha Humpohrey Polepole kitatakiwa kutoa taarifa TCRA ambapo TCRA ikijirishisha kuwa maelekzo yote yamezingatiwa kipindi cha Humphrey Polepole kitajrejea na kitakuwa chini ya uangalizi wa TCRA kwa muda wa miezi sita.

Uamuzi huu umetolewa leo jijini datr es Salaam, uamuzi wa kukata rufaa kupitia FCT upo wazi ndani ya siku 21.



from MPEKUZI

Comments