Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) anapenda kuwatangazia watu wote walioomba nafasi ya ajira ndani ya Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa kwamba mtihani wa usaili wa maandishi (apptitude test) utafanyika Jijini Dodoma siku ya tarehe 8.1.2022.
Mambo Muhimu ya Kuzingatia
1. Tarehe ya usaili ni tarehe 8.1.2022 siku ya Jumamosi;
2. Kwa waombaji ambao wameomba kazi ya Afisa Uchunguzi mtihani wao utaanza saa 2:30 asubuhi siku hiyo tarehe 8.1.2022;
3. Kwa waombaji ambao wameomba nafasi ya Uchunguzi Msaidizi mtihani wao utaanza saa 6:00 mchana siku hiyo ya tarehe 8.1.2022;
4. Waombaji walioitwa kwenye usaili huu wahakikishe wanachukua tahadhari zote za kujikinga na ugonjwa wa UVIKO-19 muda wote wanaposafiri na wanapokuwa kwenye chumba cha mtihani;
5. Majina ya waombaji wote walioitwa kwenye usaili pamoja na eneo la kufanyia mtihani yanapatikana kwenye wavuti ya TAKUKURU wwww.pccb.go.tz;
6. Kila mwombaji ajaze taarifa zake binafsi kwenye fomu ambayo imeambatishwa na orodha ya majina. Fomu pia inapatikana kwenye wavuti ya TAKUKURU pccb.go.tz:
7. Fomu ya taarifa binafsi ijazwe kwa umakini na kwa usahihi. Fomu hiyo ni sehemu ya mtihani wa apptitude test, kwa hiyo mtu atakayejaza vibaya Fomu hiyo atakuwa ameipoteza nafasi ya kufaulu kwenye usaili huu;
8. Fomu hivo iwasilishwe siku ya mtihani tarehe 8.1.2022. Msailiwa ambaye hatawasilisha_Fomu_hio atahesabika kuwa ni miongoni mwa walioshindwa kwenve usaili.
9, Watakaofaulu kwenye mtihani wa maandishi ndio watakaoitwa kwenye usaili wa mahojiano (oral interview)
Imetolewa na
Mkurugenzi Mkuu,
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa
==>>BOFYA HAPA KUPAKUA FOMU NA KUTAZAMA MAJINA
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment