RPC Pwani Awaonya Vikali Waharifu Kipindi Hiki Cha Sikukuu


 NA VICTOR MASANGU,PWANI
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani Wankyo Nyigesa amesema wamejipanga vilivyo katika kipindi hiki chote cha sherehe za  sikukuu ya Christmas na mwaka mpya katika kudhibiti kabisa hali ya vitendo vya wimbi la uhalifu na uvunjifu wa amani.


Akizungumza na waandishi wa habari Ofisini kwake Kamanda Wankyo alisema kuwa katika kipindi hiki wataongeza zaidi kufanya  misako mbali mbali ikiwemo pamoja na doria za nguvu za usiku na mchana.


“Katika kipindi hiki jeshi letu limejipanga vizuri katika kila kona katika kudhibiti hali ya uharifu katika sehemu mbali mbali ikiwemo katika kumbi za starehe pamoja na maeneo ya nyumba za kulala wageni .


Wankyo alisema wamejipanga vilivyo katika kipindi hiki lengo ikiwa ni kuhakikisha hali ya amani na utulivu inakuwepo katika kipindi chote cha sikukuu hizo na kwamba ulinzi utaimarishwa katima nyanja zote.


Pia aliongeza kwamba katika msimu huu wananchi wanatakiwa kuwa makini na watu ambao wana nina mbaya ya kuleta uvunjifu wa amani na kuwaomba wasisite kutoa taarifa kwa vyombo vya dola endapo watabaini kuwepo kwa waharifu au vurugu zozote.


Kadhalika aliwataka madereva wote wa mabasi ya kubeba abiria pamoja na Yale magari binafsi kuhakikisha wanazingatia sheria za usalama wa barabarani ili kuepusha ajali ambazo hazina ulazima wowote.


Wankyo katika kipindi hiki yeye pamoja na wasaidizi wenzake watakuwa wanafanya kazi usiku na mchana na kutoa tahadhari kwa madereva ambao wanaendesha uku wakiwa wametumia kilevi na kuwaonya kuachana na tabia hiyo.


Katika hatua nyingine aliwataka wananchi wote kusherekea kwa Hali ya amani na utulivu na kwamba Askari wake wamejipanga kwa ajili ya kuwalinda wao na mali zao.



from MPEKUZI

Comments