Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa viongozi wafuatao;
1.Amemteua Prof. Othman Chande Othman kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS).
Prof. Othman anachukua nafasi ya Dkt. Fenella Ephraim Mukangara ambaye uteuzi wake umetenguliwa. Prof. Othman ni Mhadhiri Mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
2. Amemteua Dkt. Aggrey Kalimwage Mlimuka kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Ushindani (FCC).
Dkt. Mlimuka anachukua nafasi ya Prof. Humphrey P.B. Moshi aliyemaliza muda wake. Dkt. Mlimuka ni Mkurugenzi Mstaafu wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE).
3. Amemteua Dkt. Andrew Yona Kutua kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Taifa ya Utafiti ya Magonjwa ya Binadamu (NIMR).
Dkt. Kutua anachukua nafasi ya Dkt. Deudatus Mtasiwa ambaye amemaliza muda wake.
Uteuzi wa viongozi hao umeanza Desemba 23, 2021.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment